STAA wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘ Mainda ’
amefunguka kuwa miongoni mwa vitu
vilivyokuwa vimeuteka ujana wake ni pamoja
na matumizi ya mkorogo ambapo ilikuwa
vigumu kuacha baada ya kuokoka.
Staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘ Mainda ’ .
Akipiga stori na paparazi wetu, Mainda
alisema kutokana na starehe za ujana pamoja
na kutaka kuonekana mrembo , alitumia
vipodozi hatari bila kujua kwamba vina
madhara makubwa mwilini mwake .
“ Kusema kweli niliamini mkorogo ni kitu
ambacho kingeniongezea mvuto kwa kiasi
kikubwa , bila kujua kuwa nilikuwa
najisababishia madhara mwilini.
Pia nilikuwa nafanya kitu kisichompendeza
Mungu, katika kujitakasa na maovu yangu kwa
Bwana ndiyo maana nikaamua kuacha kabisa
kujichubua japo haikuwa rahisi, ” alisema
Mainda .