Featured Posts

Tuesday, June 3, 2014

UPDATES: MAITIA MTOTO ALIYEISHI KWENYE BOKSI YAGOMBANIWA

MVUTANO mkubwa umeibuka juu ya wapi azikwe marehemu Nasra Mvungi, mtoto aliyeishi ndani ya boksi kwa miaka minne baada ya kufariki dunia hivi karibuni katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Mwili wa mtoto Nasra Mvungi ukishushwa kwenye gari ndani ya Uwanja wa Jamhuri Morogoro kuagwa.
Habari zilizopatikana mjini hapa, zinasema kuwa mzozo umeibuka kwa ndugu wa marehemu Nasra ambapo baba yake mzazi, Rashid Mvungi na bibi wa marehemu, Asha Abdallah (mama mzazi wa mama wa marehemu ambaye pia ni marehemu) kila mmoja akitaka kuuchukua mwili wa Nasra na kuuzika.
Nasra Mvungi, enzi ya uhai wake.
“Mjukuu wangu nina uchungu naye sana, nakumbuka mengi sana kuhusu yeye. Nataka kumzika mwenyewe. Hapa nilipo nimeshaagiza maturubai kwa ajili ya kuweka msiba nyumbani kwangu,” alisema Bi. Asha kwa masikitiko.
Mwili wa mtoto Nasra Mvungi ukiwa tayari kuagwa Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Risasi Mchanganyiko liliwasiliana na Ofisa Ustawi wa Jamii, Mkoa wa Morogoro, Osward Ngungamtitu na kumsimulia kuhusu mvutano huo wa kifamilia, ambapo alisema wao kama chombo cha serikali ndiyo wanaohusika na msiba huo.
“Sasa hivi (juzi Jumatatu saa 7 mchana) tunapita  Chalinze, tunakuja na maiti huko Morogoro. Sisi kama serikali kwa kuwa ndiyo tuliosimamia  matibabu ya Nasra, sisi ndiyo tutasimamia pia maziko yake. Wanatofautiana bure tu.
Nasra Mvungi enzi ya uhai wake akiwa na baba yake mzazi Rashid Mvungi.
“Tutafikisha maiti mochwari hapo Hospitali ya Mkoa halafu ataagwa katika Uwanja wa Jamhuri kabla ya mazishi siku hiyohiyo (jana).”

TUMEAMIA HUKU