Mwili wa Marehemu Mzee Small ukihifadhiwa kwenye nyumba yake ya milele jioni ya leo katika makaburi ya Tabata Segerea jijini Dar.
Msanii wa kundi la Vichekesho Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya 'Masanja Mkandamizaji',akiweke udongo kwenye kaburi la mzee Small.
Mdogo wa marehemu mzee Small akiwa chini baada ya kuzidiwa na kuishiwa nguvu muda mfupi baada ya shughuli za kuhifadhi mwili wa kaka yake kumalizika.
Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (mwenye tai na miwani katikati) akiwa na baadhi ya wasanii waliofika kwenye maombolezo.
Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Nyerere, na mtoto wa marehemu Mahmoud (aliyevaa kibaraghashia).
UMATI wa watu umejitokeza katika kumuaga marehemu Said Ngamba 'Mzee Small' nyumbani kwake Tabata-Kimanga na mazishi kufanyika katika makaburi ya Segerea, jijini Dar es Salaam.