Featured Posts

Thursday, May 8, 2014

SNURA AINGILIA KATI BEEF LA WEMA SEPETU NA KAJALA

  MSANII wa filamu na muziki, Snura Mushi ameingilia kati ugomvi wa wasanii wenzake, Wema Sepetu na Kajala Masanja na kuwaagiza wamalize tofauti zao.

Wasanii hao ambao wameingia kwenye bifu la kufa mtu kufikia hatua ya kuanikana kwenye vyombo vya habari huku chanzo kikubwa kikitajwa ni shilingi milioni 13 ambazo Wema alimlipia Kajala kama faini ya kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa rehani kisheria iliyokuwa ikimkabili mahakamani.

Nyumba hiyo iliwekwa rehani kutokana na mume wa Kajala, Faraja Agustino kushitakiwa kwa kosa la kutakatisha fedha haramu.

Snura amewataka Wema na Kajala kutoangalia nani ana makosa, wamalize tofauti zao.
“Nawashauri wenzangu wasigombane na kuwekeana vinyongo hiyo ni kama wanawapa watu faida,

nawaomba wamalize kwani haipendezi kabisa kwa jinsi walivyokuwa wameshibana. Kama mmoja anaona amemkosea mwenzake ajishushe na kuomba msamaha,” alisema Snura.
By Na Chande Abdallah na Mayasa Mariwata GPL

TUMEAMIA HUKU