Mwalimu mkuu wa shule moja ya upili nchini Uingereza ameachishwa kazi kufuatia utata kuhusu kanda ya ngono inayodaiwa kurekodiwa shuleni humo.
Mwenyekiti wa bodi ya shule alimwachisha kazi mwa muda mwalimu mkuu Graham Daniels na mfanyakazi mwingine wa shule ambaye jina lake halikutajwa baada ya malalamiko kutolewa kuwahusu wawili hao.
Hata hivyo wakuu wa bodi walisema kuwa shughuli za masomo zinaendelea kama kawaida.Kuachishwa kazi kwa mwalimu huyo kulitokea baada ya wanafunzi kusambaza kanda hiyo kwa mitandao ya kijamii. Kanda hiyo ilikuwa na sauti za watu wawili wakijihusisha na ngono katika chumba kimoja cha shule hiyo.
Mkuu wa bodi alisema: "shule imepokea malalamiko ambayo hayakumtaja mtu yeyote lakini kufuatia madai hayo uchunguzi utafanywa.''
Mwalimu mkuu na mfanyakazi mwingine wa shule wameachishwa kazi kutokana na madai hayo