Featured Posts

Friday, May 9, 2014

Mjamzito Anaswa Akijiuza Usiku wa manane Siku 3 kabla ya Kujifungua Huko Mbagala..Hii ni Laana..!!

MJAMZITO1

MJAMZITO

Mjamzito aliyejitambulisha kwa jina moja la Hamisa amenaswa laivu na ‘makachero’ wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers,  akijiuza huku akiwa na ujauzito wa miezi nane na siku 27, zikiwa zimesalia siku tatu afikishe miezi tisa tayari kwa kujifungua.
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri wiki iliyopita usiku wa manane Mbagala-Zakhem, Dar, wakati OFM ikiwa katika oparesheni zake kwenye danguro moja maarufu linalojulikana kwa jina la Kwaswai lililopo maeneo hayo.
OFM ikishirikiana na polisi wa Kituo cha Mbagala-Kizuiani ilifumuafumua danguro hilo na kuwanasa watu kadhaa wakifanya vitendo haramu na hatarishi vya ngono lakini kilichowastaajabisha na kuwaacha midomo wazi watu waliofurika katika eneo hilo, ni mmoja wa machangu hao kunaswa akiwa na ujauzito.
Mjamzito
Mjamzito Akipandishwa Kwenye Karandinga

SABABU ZA KUJIUZA.

Akizungumza na OFM baada ya kuulizwa sababu za kujiuza akiwa katika hali hiyo, mjamzito huyo alisema hayo yote yanatokana na ugumu wa maisha kwani alipata mimba akiwa katika kazi hiyohiyo.
Alipoulizwa ujauzito wake una umri gani alidai kuwa bado siku tatu tu itimie miezi tisa akajifungue.
Aliongeza kuwa kwa sasa mmiliki wa danguro hilo amemkataza kujiuza katika danguro lake kwa kuwa angeweza kujisababishia matatizo hivyo aliamua kufanyia biashara zake nje ya danguro hilo.
“Mbona mnanikamata jamani! Mimi sihusiki na danguro hilo la…(akimtaja mmiliki) kwanza ameshanikataza kujiuza kwenye danguro lake kutokana na hali yangu. Yote ni maisha tu jamani!” alisema.

Mjamzito Apandishwa kwenye karandinga.

Baadaye Hamisa(Mjamzito) pamoja na wenzake walipandishwa kwenye karandinga na kupelekwa kituo cha polisi Mbagala-Kizuiani wakisubiri sheria ichukue mkondo wake kwani shitaka kubwa linalowakabili ni uzururaji.
CREDIT: GPL

TUMEAMIA HUKU