Featured Posts

Tuesday, May 13, 2014

majanga: Wachimba mgodi 157 wafa Uturuki

157 wameaga dunia katika mkasa wa moto ndani ya mgodi
Mlipuko katika mgodi wa makaa ya mawe magharibi mwa Uturuki umesababisha vifo vya zaidi ya wachimbaji migodi 150 na kujeruhi wengine zaidi ya 70 kwa mujibu wa maafisa nchini humo.
Meya wa eneo la Manisa, Cengiz Ergun, ametoa tahadhari kwamba idadi ya watu waliokufa bado haijathibitishwa rasmi.
Inahofiwa kuwa wachimbaji mgodi wengine wengi bado wamefukiwa chini ya mgodi huo.
Inakadiriwa kuwa wakati mlipuko huo ulipotokea wafanyikazi 580 walikuwa ndani ya mgodi huo japo inaaminika wengi waliweza kukimbilia usalama wao .
Bado idadi ya walionaswa ndani ya mgodi huo haijabainika.
Mgodi huo uko katika mji wa Soma, mkoani Manisa , takriban kilomita 250 kusini mwa Istanbul.
157 wameaga dunia katika mkasa wa moto ndani ya mgodi
Jamaa za wachimbaji migodi hao wamekusanyika katika makundi karibu na mgodi huo ambao unamilikiwa na wawekezaji wa kibinafsi huku wengi wao wakilia hadharani na kububujikwa na machozi.
Waziri wa nishati Taner Yildiz ameimabia televisheni ya Uturuki kuwa huenda wengi wamekufa kutokana na sumu ya gesi aina ya carbon monoxide.
Amesema moto huo umesababishwa na hitilafu ya umeme.
Picha za televisheni zinaonyesha maafisa wa uokoaji wakiokoa wafanyikazi wa mgodi huo, huku nyuso zao zao zikiwa zimejaa vumbi.

Baadhi yao wanaweza kutembea na wengine wanabebwa na kupelekwa ndani ya magari ya kubebea wagonjwa yaliyoegezwa karibu na eneo la tukio

TUMEAMIA HUKU