STAA wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ambaye aliwahi kutangaza kuacha fani ya maigizo na muziki amejikuta akiumbuka kwa mashabiki wake kutokana na kuendelea kukomaa katika gemu kwa kuachia kazi mpya na kuandaa matamasha mbali mbali.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Baby Madaha alisema hawezi kupinga kama alizungumza hayo isipokuwa tangu atoe kauli hiyo amejikuta akizidi kupata mafanikio makubwa katika muziki.
“Naweza kusema nimeumbuka kwa kile nilichoongea, maana nimejikuta nashindwa kutekeleza nilichowaambia mashabiki wangu sababu dili zinakuja, siwezi kuziacha,” alisema Baby.