Featured Posts

Friday, July 4, 2014

UPDATES: UNAAMBIWA JOHARI,CHUCHU HANS..... TID MNYAMA NA RAY C WATIFUANA...MADAWA YA KULEVYA YAHUSISHWA, RAY C AMWAGA CHOZI,JOHARI KINGANGONI....YANI ISHAKUWA SOO


MTIFUANO! Mastaa wawili wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ na Chuchu Hans wameendeleza ligi ya bifu lao baada Chuchu kujibu mapigo huku malejendari wengine wawili wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ na Khaleed Mohamed ‘TID Mnyama’ wakitifuana.


Staa wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
JOHARI, CHUCHU
Kwa muda mrefu Johari na Chuchu walidaiwa kuwa kwenye gogoro kubwa kisa kikisemekana ni penzi la mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’.


CHUCHU AVUNJA UKIMYA
Safari hii Chuchu ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu, ameibuka na kujibu yale yote anayodai yalikuwa yakisemwa vibaya juu yake, mhusika mkuu akiwa ni Johari.
Moja ya tuhuma aliyodai kupachikwa na Johari ni ile ya kwamba amekuwa akitumia vifaa vya Kampuni ya RJ Productions inayomilikiwa na Ray na Johari.

CHUCHU ADAI KUFUATA PENZI
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum juzi jijini Dar, Chuchu alifunguka kwamba huwa anakwenda RJ kufuata mapenzi na si kampuni kwani ana uwezo wa kuwa na kampuni kwa sababu vifaa anavyo na Ray alimkuta akiwa navyo.


Staa wa sinema za Kibongo, Chuchu Hans akipozi.
JOHARI AITWA OLD FASHION
Chuchu ambaye kwa sasa anaonesha mahaba niue kwa Ray alisema kuwa anamshangaa Johari kusema kuwa anatumia vifaa vya RJ na wengine kusema ni mke mwenzake wakati Johari ni ‘old fashion’ kwani aliachwa na Ray kama wanawake wengine na yeye akaingia.

BOFYA HAPA KUMSIKIA CHUCHU LAIVU
“Mimi ndiyo ‘new fashion’, Johari atabaki kuwa ‘old fashion’ kwa Ray, sipendi kabisa watu waseme eti ni mke mwenzangu, mbona alishaachwa siku nyingi? Ukewenza unaingia vipi hapo jamani?” aliwaka Chuchu.

Chuchu aliendelea kutiririka kuwa kamwe hawezi kutumia vifaa vya RJ kwani vya kwake vinamuwezesha kufungua kampuni yake.

JOHARI ANASEMAJE?
Baada ya Chuchu kuwaka vya kutosha, kama ada ya Magazeti ya Global kutafuta mzani wa habari, Johari alitafutwa na kumwagiwa kile alichosema mwenzake ambapo aliomba aachwe kwanza kwani kwa wakati huo alikuwa kwenye kikao kizito akiomba kumpigia mwandishi baada ya kikao.
Baadaye alipopatikana alisema kwa kifupi; ‘No comment’ huku shosti wake wa karibu aliyeomba hifadhi ya jina lake akieleza kuwa, hali si nzuri kwani kuna msuguano mkali wa chini kwa chini.

Staa mkongwe kwenye muziki wa Bongo Fleva, Ray C.
NINI KIMETOKEA?
Miezi kadhaa Johari na Chuchu walidaiwa kutibuana kisa kikielezwa kuwa ni penzi la Ray ambapo mwigizaji mwenzao, Ruth Suka ‘Mainda’ ambaye naye alikuwa mmoja wa wapenzi wa kaka mkubwa huyo, yeye alikaa pembeni na kumwachia Mungu kisa cha yote kikidaiwa ni wivu wa mapenzi.

RAY C, TID
Wakati nyumba ya jirani Bongo Movies kukiwaka mto huo, kwenye muziki wa Bongo Fleva, Ray C na TID Mnyama wanadaiwa kuingia vitani kwa kisa cha kuchekesha.
TID ambaye ni mmiliki wa Top Band ndiye aliyeanza kumuwakia Ray C kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya mwanadada huyo kumuomba wazungumze.

MADAWA YA KULEVYA YATAJWA
Ilidaiwa kwamba TID ambaye amekuwa akituhumiwa kujihusisha na matumizi ya ‘unga’ huenda alihisi Ray C alitaka kumletea habari za kumsaidia kuachana nayo kupitia dawa za Methadone.
“Njoo tuzungumze TID, wewe ni Msanii Bora Afrika Mashariki, tafadhali tuzungumze tidmnyama,” aliandika Ray C.

Mmiliki wa Top Band, TID Mnyama katika pozi.
RAY C HAKUFAFANUA
Pamoja na kwamba Ray C hakufafanua kile alichotaka kuzungumza na TID baada ya kuandika maneno hayo na kuweka picha ya TID inayotambulisha Refix ya wimbo wake wa Asha, jamaa alianza kuporomosha matusi akimtaka aachane naye kabisa.

BOFYA HAPA UMSIKIE TID
“(tusi) niache mwenyewe, mimi siyo type yako. Pia sitaki kusikia chochote kutoka kwako. Makosa yako ni ya kwako, nakuomba kaa mbali (tusi) na mimi, kamsaidie boyfriend wako, sijawahi kuvutiwa na wewe, nukta,” aliandika TID kwa hasira.

MATUSU MWANZO-MWISHO
Baada ya hapo ndipo zikaibuka kambi mbili, ya upande wa Ray C ilikuwa ikimtukana TID kutokana na kile alichomjibu Ray C ambaye hakutaja nia ya kutaka kuzungumza na TID.
Kuona hivyo, nayo timu ya mashabiki wa TID ilijitoa kimasomaso na kumshambulia Ray C kwa maneno makali kama hayo aliyoyatumia TID yakipambwa na matusi.

Gazeti hili lilipomtafuta TID, mbali na matusi alikuwa na haya ya kusema:
“Mimi kama kuna mtu ananitafuta, hawezi kunitafuta kwenye Instagram, sijawahi kuwa na matatizo na Ray C.


Ray na Chuchu katika pozi.
“Kwanza sijamuona, nina kama miaka mitano hivi.
“Hivi Ray C anataka kukutana na mimi? Anataka kuongea na mimi? Mbona hajanitafuta miaka yote, ananitafuta sasa hivi? Mimi sijapenda, mwambieni sitaki kuonana naye.
“Nasema sitaki kuongea naye, sitaki kukutana naye, akaongee na maboyfriend wake ambao anafanya nao vitu vibaya, mimi si wa aina yake, aniache na familia yangu, aniache na mama yangu.”

RAY C AMWAGA CHOZI
Baada ya kushuhudia tafrani hiyo, gazeti hili lilimtafuta Ray C ambaye alionesha kusikitishwa na kile alichokisema TID hasa matusi.
“Niliona nimuombe kuonana naye na wala sikusema nilichotaka kumwambia. Nimesikitishwa na namna TID alivyonielewa vibaya.

“Nimeshamtafuta sana hadi kwao ikashindikana, kuna siku nilikutana naye Mwananyamala hospitalini, alikuwa anaumwa, nikamuomba tuongee lakini ilishindikana.
“Nilikuwa simtafuti kwa ubaya, nilitaka aje ofisini tuzungumze, nilitaka tufanye shoo ya pamoja mimi, yeye na Chidi Benz (Rashid Makwilo). Nilitaka tufanye hivyo ili kukemea matumizi ya madawa ya kulevya kwa sababu ni janga la kitaifa.

“Kweli ameniumiza kwa sababu sikuwa na lengo baya hata kidogo, sijawahi kumkosea TID,” alisema Ray C huku akimwaga machozi hivyo mwanahabari wetu akamuomba anyamaze.
Kwa sasa Ray C anaendesha kampeni ya kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya kupitia taasisi yake ya Ray C Foundation ikiwa na slogani ya Tanzania Bila Madawa ya Kulevya Inawezekana.

KUTOKA KWA MHARIRI
Hivi karibuni waigizaji Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja walimaliza tofauti zao hivyo ni vyema wasanii hao nao wakamaliza bifu zao.

TUMEAMIA HUKU