Wakati sheria ikizidi kuwatia hatiani wale nguli wa kulawiti watoto, staa wa bongo movie, Jackline Wolper amesema kuwa hata kwa upande wake huwa anasikitishwa na vitendo hivyo kwani kufanya hivyo ni kuwatia doa katika maisha yao......
Staa huyo alisema kuwa kitendo cha kulawiti mtoto ni cha kinyama na kwamba haoni sababu ya kucheka na watuhumiwa bali wanatakiwa kufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake...
"Kuna watoto wanalawitiwa na kubakwa huko vijijini na hata hapa mjini, lakini unakuta wazazi wanazungumza nyumbani na kuyamaliza bila kujua yule mtoto ameathirika kiasi gani, inauma sana, ni lazima wafikishwe mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake",alisema Wolper