Na Gabriel Ng’osha/GPL
KUFUATIA mtandao wetu wa www.globalpublishers.info kuandika habari iliyokuwa inasema “Watoto njiti mapacha watelekezwa na baba yao’’, hatimaye Wasamaria wema wajitokeza kumsaidia mama wa watoto hao, Fatuma, ambaye amezaa mapacha Rahma na Rahmu.
Akizungumza na mwandishi wetu leo alisema: ‘’Naishukuru sana kampuni ya Global Publishers kwa kuyatangaza matatizo yangu pia namshukuru sana dada Mary Chibwana kwa kujitolea kunipatia fedha kwa ajili ya mahitaji ya watoto. Vilevile nawashukuru wote walionisaidia kwa fedha, salamu na hata ushauri.”