Featured Posts

Wednesday, July 2, 2014

KUFA KUFAANA: BAADA YA SUAREZ KUFUNGIWA MIEZI MINNE, TIMU ZA MGOMBANIA KISA NCHI ZAO HAZITAMBULIKI NA FIFA KWA HIYO ANAWEZA KUCHEZA

Ruis Suarez akishangilia bao

kweli kufa kufaana , baada ya mchezaji luis suarez kufungiwa kujihusisha na mpira au michuano yoyote ambayo iko chini ya fifa kwa kipindi cha miezi minne, club moja ndogo huko ya Hajvalia huko  kosovo ambayo kwa uhalisia uwezi kuifananisha na yanga wala simba kwa hapa kwetu tanzania, imejitokeza na kutangaza ofa kwa mchezaji huyo hili akacheze katika club yao kwa kipindi chote ambacho atakua akitumikia kifungo chake, akizungumza katika vyombo vya habari direkta wa timu hiyo Xhavit Pacolli, anasema " Suarez hawezi kucheza kwa miezi minne ijayo na sisi hatuko fifa , nadhani anaweza kucheza hapa Kosovo kwa hiyo tuna ofa ambayo tutaituma liverpool" hata hivyo kiwango ambacho wamesema watamlipa ni kichekesho ukilinganisha na ubora wa mchezaji huyo,  lakini direkta huyo alikiri kuwa ndio uwezo walio nao. 

TUMEAMIA HUKU