Tayari
mpaka sasa abiria zaidi ya 300 wamepoteza maisha kwenye ajali tatu za
ndege zilizotokea ndani ya wiki moja kuanzia wiki iliyopita ambazo ni
ndege ya Malaysia, nyingine huko Taiwan na nyingine iliyoanguka Mali.
Matukio ya ndege yanaendelea kukaa kwenye wino wa vichwa vya habari
baada ya hili jingine la ndege ya Sunwing ambayo ililazimika kukatisha
safari na kurudi ilikotoka baada ya maneno ya kijana wa miaka 25 raia wa
Canada kuongea na muhudumu wa ndege na kusema anataka kuilipua Canada.
Ndege hiyo iliyoruka saaa moja asubuhi Ijumaa July 25 2014 ikiwa na
abiria 181 kutokea Toronto Canada kuelekea Panama City ambapo kijana
huyu aliongea na Muhudumu aliekua anapita na kumwambia jinsi sigara
zilivyo bei ghali nchini Canada na kwamba anaichukia nchi hiyo.
Baada ya hapo kijana huyu aliongea kwa kujiamini na kwa sauti ya msisitizo na ishara za mikono kwamba anataka kuilipua Canada.
Muda
mfupi baada ya hiyo kauli Muhudumu wa ndege alitoa taarifa na ndege
hiyo ikaamrishwa kugeuza kurudi ilikotoka wakati huohuo pia ikiwa
inasindikizwa na ndege mbili za kivita zilizopewa amri kuifatilia zikiwa
zinafaya mazoezi.
Baada ya kutua tu saa mbili na dakika 55 ikabidi Polisi waingie ndani
wakiwa na silaha na kumchukua kijana huyu aitwae Ali Shahi na kuanza
kumuhoji hapohapo uwanja wa ndege ambapo alitarajiwa kupelekwa
Mahakamani saa tatu kamili asubuhi.
Hata
hivyo baada ya taarifa kuenea, baba wa huyu mtoto amejitokeza na kusema
mwanae amekua na matatizo ya akili toka akiwa na umri wa miaka 16 hivyo
alichosema hakuwa anamaanisha.
Milioni 392 Zajenga Barabara HEWA Dar es Salaam
-
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob amebaini matumizi ya Sh392
milioni zilizoandikwa kwenye taarifa ya manispaa hiyo kuwa zimetumika kwa
ajili y...