Featured Posts

Monday, July 14, 2014

HUYU MCHUNGAJI AAMBIWA NA MUNGU KUHAMIA MAREKANI, ASEMA AKITAJIRIKA ASIITWE WA SHETANI


Mchungaji wa Malawi mwenye makazi huko Afrika ya kusini Hastings Salanje ambaye amekuwa akipamba vichwa vya habari nchini kwake, amewaambia Wamalawi kwamba wasije kumwita mtu wa shetani endapo atakuja kuwa tajiri.

'' Nitafanya kile ambacho Mungu ameniambia na kwenda kule anakotaka mimi kwenda, kwa watu wanaonipenda naomba mniombee kwasababu hii sio kwa ajili yangu pekee bali pia kwa watu wa Mungu , kwa wote mnaonichukia nawaambia hamuwezi kuzuia mbingu lakini mbingu inaweza kuwazuia, nawaambia yote haya ili itakapokuja kutokea kesho msije kuniita mtu wa shetani nawaambia sasa si mbali yote haya karibia yanatimia naamini Mungu alikuwa ananiandaa mimi kwa ajili ya hii''.

Mchungaji Salanje ameyasema hayo wakati akihojiwa na gazeti la Nyasa Times ambako ameweka wazi kwamba ana mpango wa kuhamishia huduma yake huko nchini Marekani kama alivyoambiwa na Mungu kufanya hivyo kwani atakuwa tajiri. mchungaji huyo ambaye alianza kuwa maarufu mwaka 2003-2004 nchini kwake Malawi kabla ya kuhamia Afrika ya kusini kutokana na miujiza yake ya uponyaji akiwa pia akijulikana kupitia wimbo wake maarufu uitwao ''Yenda Iwe'' ambao huutumia wakati wa uponyaji.

Maagizo ya kuhamia nchini Marekani ameyapata mwaka jana mwezi April kwamba Mungu anamtaka ajitayarishe kuhamia New York akawa kama amechanganyikiwa kwakuwa hakutarajia alichoambiwa hivyo kuingia kwenye maombi kwa siku tatu ambapo siku ya tatu Mungu akampa maono ya watoto wakipeperusha bendera ya Marekani wakiwa katika moja ya ukumbi .

Amesema Roho mtakatifu ndio amemwambia kuhamia nchini Marekani na sio kama watu wanavyodhani, akaenda mbali zaidi na kukumbushia kuwa mwaka 1996 Mungu alipomwambia anataka kumtumia alihama mwaka 1999 kutoka Ntcheu hadi Blantyre ambako Mungu alimwambia afungue huduma yake ambapo mwaka 2003 akaanza kuzunguka kuhubiri injili sehemu mbalimbali Malawi ikiwemo Zomba, Lilongwe na Blantyre ambapo mikutano yake ikaanza kuonyeshwa katika TV Malawi na sasa MBC TV.

Akiwa Blantyre Mungu akamwambia aende Mzuzu ambako akiwa katika chumba cha hotel Mungu akampavision ya uwanja wa ndege, ndege zikipaa na kutua akiwa anaangalia majengo ya ule uwanja sauti ikamwambia nakuchukua mpaka mjini, anasema aliporudi Blantyre alikuwa na maombi ya kufunga ili Mungu kumuonyesha kile alichokuwa akimuonyesha kwenye ndoto akiwa Mzuzu ndipo Mungu akamfunulia kwamba ajiandae kuhama Malawi na kumfuata yeye lakini anasema alipowaambia Wamalawi hawakumuelewa zaidi ya kumsema vibaya kuhusiana na uamuzi wake.

Akiwa Afrika ya kusini Mungu akaanza kumuonyesha mafunuo ya kumiliki mambo mengi zikiwemo ndege, mali,makampuni makubwa, makanisa na mambo mengine mengi huku Mungu akimwambia atamkabidhi hivyo vitu (Mungu mwenyewe ndiye atampa mchungaji Salanje), anasema mda mwingine anamuona Yesu kabisa akimshika mabega yake na kumwambia amefanya miujiza yote (Yesu) nchini Malawi akiwa mbinguni lakini sasa atakuwa anakuja yeye mwenyewe kuitenda.atakuwa na uwezo wa yeye tu( mchungaji) kumuona Yesu wengine hawataweza, '' hata sasa nimeshawaona malaika mara nyingi nikiwa naendesha gari na mwaka 2009 akanionyesha ninamna gani naweza kuwekeza na kupata mabilioni ya pesa. kwa siku tatu Roho Mtakatifu anaweza akaja kwa siku tatu kunifundisha namna ya kuwekeza Mungu amenipa hekima na siri ya namna ambayo wengine hawana ni maeneo gani naweza kuwekeza nitakuwa wakwanza kuzalisha elimu niliyopewa na nitazalisha pesa nyingi, nina uhakika wa kuwa Bill Gates wa Afrika''.

Soma mwendelezo wake kwa lugha ya kiingereza kama ilivyoandikwa na gazeti la Nyasa Times la Malawi juzi;-

At the same time I could see myself holding the same flag and doing what they were doing. I also saw something in a womb of a woman and beside it there was a USA flag and the Lord said that He saw me holding same flag in my mother’s womb, when I went to school and even when I preached in Malawi I was holding same flag. Then He told me that I shouldn’t be confused but rather get ready to go there.  

When I started researching, I found out that if I can invest in USA, I can make more money than in RSA. What I can make in USA, in RSA is just 3% of that. Because in a year in USA I can get not less than $2billion while in South Africa I can’t make more than R400 a year. While in USA, I will be able to invest in Canada, Australia, Europe and RSA. In terms of gospel, I can reach out to a lot of people in USA than in RSA. I only need R500 to achieve all these,” said the pastor. 

 “So you see if I had disobeyed God and stayed in Malawi I would have missed all these and suffer in Malawi like many people. I dint run away from Malawi because I wronged no one there and I have visited the country several times since I came here. It’s just that most Malawians have got small minds. They are easily satisfied with small glory.

He also said that his plans are to help build Malawi financially.

My plans for Malawi are to build my country both spiritually and financially. I want to create jobs, build churches and houses for poor people in Malawi and I believe God will make me achieve this,” concluded the Pastor.

Hastings Salanje was born on 28 August 1972 and is married to Jennet Salanje and has six children together, five boys and a girl. He became born again in 1991 and received calling in 1996.

TUMEAMIA HUKU