Ishu ilikuwa hivi, kuna gari ndogo ilikuwa inatokea njia ya Kawe kwenda Shopperz au ilikuwa inaelekea mjini kwa kutumia hii njia ya Mwai Kibaki road.
Hiyo gari ndogo ilipofika Maeneo ya Million Hairs Salon jirani kabisa na Regency park hotel ikakwama kwenye foleni ndefu sana,nyuma ya hiyo gari ndogo kulikuwa na magari mengine yameunga hiyo foleni.Gari ya magereza ikiwa na wafungwa ilikuwa ni kama ya sita au ya nne nyuma ya hiyo gari ndogo mara ghafla tukasikia puu puuu poo pooo kama risasi 6 au 8 hivi,kumbe ile gari ndogo inavyosemekana ilikuwa imebeba kiasi kikubwa cha pesa na hakukuwa na escort yoyote.
Majambazi wakiwa kwenye pikipiki waliifuata ile gari pale kwenye foleni wakamuamrisha yule jamaa atoe fedha na jamaa akaachia mkwanja.
Sasa lile gari la magereza kwa vile liko juu sana kama gorofa askari wake wakaiona hiyo inshu live,sasa ile wanajiandaa tu na mabunduki yao' majambazi nayo wakashitukia mchezo na wakaanza wao kuwashambulia kwa risasi wale askari magereza.Askari magereza ile wanajiandaa kujibu mapigo tu majambazi haooooo wakawasha pikipiki na kuondoka kwa speed ya 220.
Kiukweli ilitisha na watu waoga kama mimi nilikimbilia kujificha sehemu,yaani ilikuwa kama Movie.
Basi la magereza lililoshambuliwa likiwa eneo la tukio.
Milioni 392 Zajenga Barabara HEWA Dar es Salaam
-
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob amebaini matumizi ya Sh392
milioni zilizoandikwa kwenye taarifa ya manispaa hiyo kuwa zimetumika kwa
ajili y...