Featured Posts

Monday, September 1, 2014

URAIA WA NCHI MBILI WAENDELEA KUPINGWA NA WAJUMBE BUNGE LA KATIBA

la uraia pacha limeonekana ‘kupigwa
chini’ na serikali na wajumbe wa Bunge
Maalumu la Katiba baada ya wote
kukubaliana zaidi juu ya hasara za
kuruhusu uraia huo, ikiwemo hofu ya
usalama wa taifa na uzalendo kupungua.
Katika semina iliyoandaliwa kwa
Wajumbe wa Bunge hilo na mada
kutolewa na Idara ya Uhamiaji, Abdallah
Khamis Abdallah ambaye ni Kamishna wa
Udhibiti na Mipaka wa idara hiyo,
imeonesha kuruhusiwa uraia pacha ni
hasara zaidi kwa Tanzania kuliko faida.
Suala hilo kwenye semina hiyo
likawafanya wajumbe zaidi ya 12 kati ya
16 waliochangia kukataa uraia pacha na
kumuacha mwakilishi wa Diaspora,
Kadari Singo kutumia nguvu nyingi
kutetea uraia pacha huo.
Wajumbe wa Bunge wakizungumza na
mwandishi wameeleza kuwa Uhamiaji
imeeleza kuwa Watanzania wameondoka
nchini kwa sababu za kufuata elimu,
viapo vilivyowafanya wawe watiifu kwa
nchi walizopata uraia na wengine kwa
kuitukana nchi haifai na hawawezi kuishi
Tanzania.
Mjumbe Wazir Rajab Salum alisema
Uhamiaji imetaja faida ya uraia pacha ni
za kiuchumi pekee na nyingi ni hasara,
ikiwemo kuangalia uzalendo ambapo
imeonekana kuruhusu kutapunguza
uzalendo na usalama wa taifa utakuwa
hatarini.
“Kumeonekana yule mtanzania aliyeapa
kuilinda nchi ya pili iliyompa uraia
mwingine ni rahisi kumtumia kuifanyia
ubaya Tanzania na walioondoka
wameonekana wanakosa uzalendo hata
akirudi hawezi kuwa sawa na Mtanzania
aliyebaki nchini miaka yote,” alieleza
Salum.
Hata hivyo, aliongeza; “wapo waliounga
mkono uraia pacha lakini wakataka
watanzania waliochukua uraia nje
wawekewe utaratibu wakipewa uraia
nchini wasiruhusiwe kushiriki nafasi za
uongozi yaani wasichague wala
kuchaguliwa”.
Naye Almas Maige alisema Uhamiaji
imeona waliokula viapo nje vya uraia
hawataweza kutumikia ‘mabwana’ wawili
na tayari wameshaonekana si waaminifu
kwa nchi yao ya awali.
Hata hivyo, Singo akizungumza na
waandishi wa habari kwenye viwanja vya
Bunge alitetea hoja yake ya Tanzania
kuruhusu uraia pacha na kusema,
“wanasema aliyeomba uraia wa nje
amekosa uzalendo hivi mzalendo ni yupi
anayeiibia pesa nchi akapeleka nje au
anayeleta pesa nchini. Uzalendo si kigezo
kwani mtu yeyote anaweza kukosa
uzalendo…”
“Usalama wa taifa wanaosema
unahatarishwa ni upi ni kwa mtanzania
aliye nje kuja nchini kwake au kumpa uraia
wa pili Mnyarwanda ambaye nchi yake
inaruhusu uraia pacha na ukamnyang’anya
hati ya kusafiria na akienda kwao atapewa
nyingine huku akitoa siri za nchi na yule
mfanyakazi wa serikali mwenye siri nyingi
anayezitoa kwa kupokea rushwa. Marekani
inaweza kuleta satelaiti ikasikiliza
mawasiliano ya nchini. Hivi si vigezo vya
kumnyima uraia mtanzania aliye nje”.
Akitoa mifano ya faida kwa nchi
zilizoruhusu uraia pacha, alisema
Wachina waliopo nje wanarudisha kwao
dola za Marekani bilioni 60 kwa mwaka,
Nigeria dola za Marekani bilioni 20 na
Kenya inapata dola za kimarekani bilioni
1.7 kutoka kwa Wakenya waliopo
Diaspora.
Kwa sasa watanzania waliopo wanaleta
nchini dola za kimarekani kati ya milioni
10 na 37 huku Benki ya Dunia ikionesha
watanzania waliopo nje ni milioni tatu.
Alishauri uraia pacha uruhusiwe na
kuwekwe mipaka, kwani hata yeye na
watanzania waliopo nje wanajua
hawawezi kurejeshewa uraia wao kwa
asilimia 100. Tanzania ni kati ya nchi saba
za Afrika ambazo hazijaruhusu uraia
pacha. Burundi ni miongoni mwao.
Katika semina hiyo Katibu Mtendaji Ofisi
ya Rais, Tume ya Mipango Dk Philip
Mpango aliwaeleza wajumbe wa Bunge
Maalumu la Katiba umuhimu wa kuweka
mpango mkakati wa uchumi imara
kwenye rasimu ya katiba mpya na
kuwekwe uhakika wa viwanda endelevu

TUMEAMIA HUKU