Imeandikwa na Malisa Godlisten
Ninaandika makala hii nikitambua bayana kuwa
itamuudhi kila mtu anayeingia mtandaoni kwa
minajili ya kuwanyanyasa wengine. Lakini siku zote
ninaamini katika busara hii: kuuchukia ukweli
hakubadilishi ukweli kuwa uongo. Ukweli ni ukweli
na uongo ni uongo. Ukweli hauwezi kuwa uongo,
na kadhalika uongo hauwezi kuwa ukweli. Kamwe
asilani. Wakati tunaomboleza kifo cha ndugu yetu
Betty Ndejembi watu wamesema mengi, na
yameandikwa mengi. Kila mmoja kwa namna
alivyoguswa. Zitto kabwe ametweet hivi asubuhi
“justice for betty”, akitoa rai haki ipatikane kwenye
kifo cha Betty.
Marehemu Betty Ndejembi
Jokate Mwegelo naye ametweet kuomba msaada
wa kuchunguza kifo cha Betty. Na watu wengine
maarufu kila mmoja kasema neno, labda kwa
sababu Betty alikuwa maarufu in one way or
another. Lakini hatuwezi kukwepa ukweli kwamba
siku chache kabla ya kifo chake, alinyanyaswa mno
kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.
Japo hadi muda huu hatuwezi kuhusisha moja kwa
moja uhusiano kati ya unyanyasaji huo na kifo
chake, lakini mtu akinyanyaswa masaa kadhaa
kabla ya kifo chake, waweza kujenga picha fulani.
Saa chache kabla ya kifo chake Betty alitweet ‘ITS
ALWAYS THE PEOPLE YOU TRUST WILL DO
THEOST DAMAGE TO YOU…ITS BEEN A GOOD LIFE
THO’.
ITS ALWAYS THE PEOPLE YOU TRUST WILL DO
THEOST DAMAGE TO YOU...ITS BEEN A GOOD
LIFE THO
9:08 PM - 26 Aug 2014
Betsy______
@BettyNdejembi Follow
32 RETWEETS 14 FAVORITES
Baada ya kutweet hakuonekana tena hadi
alipookotwa mtaroni kesho yake asubuhi akiwa
amefanyia vitendo vya kikatili na akiwa amepoteza
fahamu.
Lakini kabla hata ya kutweet hivyo, Betty alikuwa
anaandamwa sana mtandaoni huko Twitter. Kuna
watu walianzisha team ya kumtukana, kumjibu
hovyo na kumprovoke kwa kila alilofanya. Naomba
ieleweke kuwa simlaumu mtu kwa sababu sina
mamlaka ya kufanya hivyo bali dhima ya makala
hii ni rambirambi zangu kwa Betty kuzungumzia
tatizo la unyanyasaji mtandaoni, sambamba na
suala zima la unafiki kila kinapojiri kifo hususani
cha mtu maarufu. Tuna tatizo kubwa huko
mitandaoni.
Tumefika hatua ya kuwapa umaarufu watu wenye
matusi ya nguoni, wazushi, wambeya, wanafiki.
Wanaochafua wenzao, kutishia wenzao kwa
kujifanya askari jkt, kusengenya na kupost
majungu…. Aina ya binaadamu wanaostahili laana
lakini twaishia kuwatukuza.
Kwenye hii mitandao, matusi imekuwa njia ya
mkato ya kupata umaarufu. Kuna wenzetu wengi tu
wenye ‘umaarufu’ huko twitter, facebook na
instagram lakini ukidadisi chanzo cha ‘umaarufu’
huo, utaambiwa ‘ah huyu ana matusi si mchezo!’
Kuna watu wazima na akili zao wanatumia muda
mwingi kwenye mitandao ya kijamii aidha
kunyanyasa wenzao kama si kusherehesha
unyanyasaji huo. Marehemu Betty ni victim wa
yote hayo.
Alitukanwa sana, na aliitwa majina kadhaa ya
kumdhihaki kabla ya kukutana na mauti.
Kuna waliomwita Di maria, superstar uchwara etc..
and I hope hao waliomuita hivyo wanajifahamu na
wengine wananisoma hapa. Japo sijui chanzo cha
‘ugomvi’ wao, lakini naamini kuna watu wengi tu
waliokuwa katika nafasi ya kuzima moto huo kwa
vile walikuwa wakizifahamu pande zote mbili za
‘ugomvi’ husika lakini kwa sababu ya unafiki
wakapalilia moto maana wanafurahi watu
wakigombana.
La kukera zaidi ambalo ni wazi litajichomoza
wakati wa maombolezo haya ni unafiki. Watu
walewale waliodiriki kumwandama marehemu
wakati wa uhai wake watageuka kuwa wenye
uchungu mkubwa baada ya kifo chake.
Hii inanikumbusha suala ambalo nimeshawahi
kulizungumzia mara kadhaa kwamba ‘wakati
muafaka wa kutafuta vipaji vya uigizaji ni kwenye
misiba: watu walewale waliokuwa wakikuchukia
kwa nguvu zote watageuka wenye uchungu
mkubwa kwa kifo chako.’ Ukiangalia baadhi ya
tweets za mwisho za marehemu ni wazi kuwa binti
huyo alikuwa anahitaji msaada kutoka kwa
wanaomjali. Mojawapo ya tweet za mwishomwisho
za marehemu alisema hivi;
“Thank you all for the names I was called, luck
y’all have such a perfect life.! No hard feelings..
I’m alive still.! Endeleeni kuongea.” Kwa tafsiri
isiyo rasmi Betty alisema “asanteni kwa majina
yote mliyoniita. Mmebarikiwa kuwa na maisha
mazuri.! Hamuumizwi na hisia kama mimi. Ila
bado ninaishi, endeleeni kuongea.” Kwa bahati
mbaya hakuna aliyejali, hadi juzi asubuhi
(Jumatano) Betty alipookotwa kwenye mtaro akiwa
amefanyiwa unyanyasaji wa kijinsia na akiwa
amepoteza fahamu. Kifo cha Betty ni miongoni
mwa vifo vya kikatili sana kuwahi kutokea nchini.
Nashauri wanaharakati ea haki za wanawake
wapambane kuhakikisha haki inapatikana.
Akina Annanilea Nkya, Hellen Kijobisimba watafute
haki ya binti huyu kama Zitto Kabwe alivyosema
“justice for betty” imagine mtu aliyekua kwenye
maumivu makali ya hisia, anatekwa na genge la
wahuni. Bila kujali kipindi kigumu alichokua
anapitia, bila kujali hakua na wazazi, bila kujali
psychological torture aliyokua nayo still
wanamfanyia unyanyasaji wa kijinsia hadi
anapoteza fahamu.
Betty aliokotwa mtaroni na kupelekwa hospitali.
Jana (Alhamisi) aliweza kufungua macho, lakini
hakuweza kuongea lolote hadi saa 3 usiku wa
kuamkia leo, mauti ilipomkuta. Kwaheri betty,
kwaheri classmate wangu (Majengo sec). Kwaheri
rafiki, kwaheri ndugu. Umeondoka dunia bado
inakuhitaji. Naumia you have gone too young,
lakini naumia zaidi sababu umekufa kikatili mno.
Japo sijui nitakufaje, lakini nadiriki kusema
hukustahili kifo cha aina hii. Nakumbuka sms yako
ya mwisho kwangu uliniambia hivi “Malisa blv me,
only youths can change this country”. Leo
nilipopata taarifa ya kifo chako nimerudia kuisoma
sms yako mara mbilimbili.
Sikujua kuwa sms hiyo ndo ulikua unaniaga.
Umeniaga kwa kutuachia vijana wosia, kuwa vijana
pekee ndio wenye uwezo wa kuibadilisha nchi hii.
Nitakua nimekusaliti ikiwa sitautendea kazi wosia
huu. I promise to fight and motivate other youths
to liberate this country for your dedication.
Umekwenda kumfuata mama yako, umemfuata
baba yako. Wazazi wako walitangulia, leo wewe
umewafuata. Hatimaye familia nzima mmekutana
Paradiso.
Huu ni baadhi ya ujumbe uliondikwa na watu
mbalimbali waliokuwa wakimfahamu Betty;
Faraja Nyalandu
Kifo cha Betty kimetuachia mafundisho mengi.
Natumai kila mmoja aliyemfahamu Betty kwa
namna moja ama nyingine amepata lake la
kujifunza. Gharama ya mafundisho tuliyoyapata ni
kubwa sana. Maumivu. Kifo. Aliyelipa ni Betty na
wanaompenda. Itafaa gharama hii isiende bure.
Tuwe wakarimu. Tuwe na upendo. Tumshike mtu
mkono pale alipo na uhitaji. Tumnyanyue
akianguka. Lakini vyote haviwezi kuwa kama ndani
yetu havipo. Huwezi kutoa ambacho huna. Tuanze
ndani yetu. Betty tusamehe. Mungu atusamehe na
Mungu atusaidie. Pumzika kwa amani Betty.