Featured Posts

Friday, September 12, 2014

KAMA ULIKOSA PICHA JINSI KIBONDE NA GADNER WALIVYOPANDISHWA KIZIMBANI, ZOTE ZIKO HAPA

Watangazaji Ephraim Kibonde (wa pili kushoto) na mwenzake Gardner Habash (wa tatu kulia) wakielekea kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni jijini Dar. (Picha na Maktaba)
WATANGAZAJI Ephraim Kibonde wa Clouds FM na mwenzake, Gardner Habash wa Times FM leo wamepandishwa kizimbani tena katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni jijini Dar kwa kusababisha ajali, kutotii amri ya polisi na kutoa lugha ya matusi

Watangazaji hao wamesomewa mashitaka hayo na Wakili wa Serikali, Mkimbu Ramadhan mbele ya Hakimu Aniseta Wambura.

Kibonde na Gadna wanadaiwa kutenda makosa hayo Jumamosi ya Agosti 9, mwaka huu saa 12 asubuhi, katika eneo la Makumbusho, Dar ambapo Kibonde akiwa anaendesha gari walilokuwa wamepanda aliligonga gari la raia mmoja wa kigeni (Mzungu) na kukimbia.
Kesi yao imeahirishwa mpaka Oktoba 2, mwaka huu itakapotajwa tena.

TUMEAMIA HUKU