Fedha inaongea! Staa wa filamu za nyumbani, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amenunua gauni la nguvu kwa ajili ya uzinduzi wa filamu yake mpya ya Foolish Age lililomgharimu dola za Kimarekani 1,350 (zaidi ya Sh. milioni 2.16).
Kwa mujibu wa staa huyo, gauni hilo lilikuwa ni oda maalum ambapo alilivaa kwa muda kisha akabadilisha na kuvaa mengine mawili yanayofanana na hilo.