Mwanaume mmoja mkazi wa Kiseke, Ilemela jijini Mwanza amekutwa amekufa baada ya kujinyonga kwa kamba juu ya mti huku mwili wake ukiwa umeharibika vibaya na kuvuja maji….
Inakadiriwa kuwa mtu huyo alijinyonga siku tatu zilizopita na chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika kutokana na mtu huyo kutoaacha ujumbe wowote huku wakazi wa eneo hilo wakishindwa kumtambua vizuri kutokana na mwili wake kuharibika.
Kutokana na hali hiyo, maafisa wa jeshi la polisi waliokuwepo eneo la tukio waliamuru mwili huo uzikwe baada ya uchunguzi wa awali wa daktari aliyekuwepo eneo la tukio