Featured Posts

Friday, September 5, 2014

BOKO HARAMU WAWAZUIA WATU KUWAZIKA NDUGU ZAO

Taarifa za kutisha zimeibuka kutoka mjini Bama
moja ya miji ambayo ilitekwa na wapiganaji wa
kiisilamu wa Boko Haram Kaskazini Mashariki ya
Nigeria
Seneta mmoja wa eneo hilo,Ahmed Zanna,
aliambia BBC kwamba wakazi hawaruhusiwi
kuwazika jamaa wao waliouawa na wapiganaji hao.
Inaarifiwa miili imetapakaa katika barabara za mji
huo ambao Boko Haram imeuteka.
Kundi hilo linasemekana kuuteka mji huo huku
wapiganaji wa kundi hilo wakishika doria katika
barabara zake.
Maelfu ya watu wametoroka huku idadi kubwa ya
wengine wakiuawa.
Seneta huyo ameitaka serikali ya Nigeria kupeleka
wanajeshi mjini Maiduguri ambao ni mji mkuu wa
jimbo hilo ili kuulinda dhidi ya wapiganaji hao.
Mnamo siku ya Jumatano serikali ya jimbo hilo
ilikanusha madai kuwa jimbo hilo limetekwa na
wapiganaji hao.
Maafisa wakuu wanakisia kuwa watu 26,000
wameachwa bila makao kutfuatia mapigano katika
mji wa Bama.
Bwana Zanna anasema kuwa barabara za mji huo
zimejaa miili ya watu na Boko Harama imewakata
wakazi kuwazika jamaa wao. ”Kwa hivyo hali ni
mbaya na inaendelea kuzorota,” asema bwana
zANNA
Boko Haram wameteka miji kadhaa Kaskazini
Mashariki ya Nigeria, katika miezi ya hivi karibuni
na kusababisha hofu kuwa huenda wakaufikia mji
mkuu Maiduguri.
Bwana Zanna amesema kuwa itakuwa janga kubwa
ikiwa Boko Haram wataushambulia mji wa
Maidiguri ambao una watu zaidi ya milioni mbili.

TUMEAMIA HUKU