Featured Posts

Thursday, September 4, 2014

ACHOMWA MOTO AKIDAIWA KUIBA BAISKELI MOROGORO SOMA HAPA

Mwili wa kijana huyo ukiwa katika gari la polisi kupelekwa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

KIJANA anayesadikiwa kuwa kibaka na ambaye hajafahamika jina lake, leo asubuhi amechomwa moto hadi kufa akidaiwa kuiba baiskeli maeneo ya Nane Nane mjini Morogoro, jirani na shule ya Sekondari ya Alfa James ambayo ni maarufu kama Shule ya Father Pekupeku.
”Majira ya saa moja asubuhi tumeona vijana wanne wakimfukuza mwenzao, walipofika hapa kwenye mabweni ya shule ya Alfa, wakamkamta akiwa na baiskeli na kumshushia kichapo kikali na baadaye wakamchoma moto wakidai alikuwa ameiba baiskeli yao maeneo ya Tubuyu, ” alisema shuhuda mmoja ambaye alijitambulisha kwa jina la Mama Happy.

Gari la polisi likiondoka na mwili wa kijana huyo.



Mtandao huu wa paparazi ulishuhudia kijana huyo akiendelea kuteketea kwa moto akituhumiwa kuiba baiskeli kuukuu yenye thamani ya shilingi  60,000. Polisi walifika  na kuuchukua mwili huo na kuupeleka Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.


Wanafunzi wa Sekondari ya Alfa James wakishuhudia mahali alipochomewa mtuhumiwa.
Raia wengine waliofika eneo la tukio.

TUMEAMIA HUKU