HABARI kubwa ya mjini hivi sasa, hasa kwenye
mitandao ya kijamii ni juu ya madai mazito ya
kuvunjika kwa ndoa ya selebriti wawili Bongo,
staa wa muziki wa Kizazi Kipya, Judith
Wambura ‘ Lady Jaydee ’ au ‘ Jide ’ na
mtangazaji maarufu wa Radio Times FM ,
Gardner G . Habash, iliyofungwa Mei 14 , 2005 ,
Ijumaa linamaliza utata. KABLA
Kabla ya Gardner kufunguka , habari zilidai
kwamba wawili hao walikuwa kwenye gogoro
zito ambapo Gardner aliamua kuondoka katika
nyumba waliyokuwa wakiishi pamoja iliyopo
Kimara - Temboni, Dar.
Ilidaiwa kwamba baada ya kuondoka nyumbani
eti Gardner alikwenda kukaa kwa mmoja wa
ndugu zake.
Habari hizo za kwenye mitandao ambazo
hazitaji chanzo cha kuvunjika kwa ndoa hiyo ,
zilidai watu wa karibu na familia hiyo walisema
hiyo siyo mara ya kwanza kwa wawili hao
kutengana , lakini mzozo wa safari hii unaweza
ukawa wa moja kwa moja.
ACHA BWANA !
Ilidaiwa kwamba ni kutokana na kutemana
huko, ndiyo maana Jide msanii anayetajwa
kuwa ni miongoni mwa wenye mafanikio
kimaisha Bongo, hakwenda Kituo cha Polisi
Oysterbay , Dar kumwangalia mumewe ambaye
aliwekwa korokoroni kufuatia kitendo chao cha
kuwakimbia askari wa usalama barabarani
akiwa na Ephraim Kibonde hivi karibuni. MAFUMBO ?
Ilisemekana kuwa hisia za kuachana huko
zinachochewa pia na baadhi ya maandiko
ambayo mwanamuziki huyo wa Kibao cha
Yahaya , amekuwa akiyaweka katika akaunti
zake za mitandao katika siku za hivi karibuni.
Ilielezwa kwamba katika akaunti yake ya
Mtandao wa Istagram, Jide aliweka picha yake
akiwa amesimama nje ya gari lake kisha
akasindikiza kwa kuandika hivi : “ Walking away
from troubles ” , maneno ambayo kwa tafsiri
isiyo rasmi yanamaanisha kujiondoa kwenye
matatizo.
BINTI MACHOZI?
Ilidaiwa kuwa kabla ya hapo , katika mitandao
inaandikwa kuwa Jide pia aliweka picha yake
akionekana kuwa na huzuni huku Binti
Machozi akilengwalengwa na machozi na
kusindikizia na maneno akiuliza : “ Sijui
nisemaje?”
IJUMAA MZIGONI
Kufuatia tetesi hizo , gazeti hili liliamua
kuzifanyia kazi ili kupata ukweli .
GARDNER ANASEMAJE ?
Mtu wa kwanza kupigiwa simu alikuwa ni
Gardner ambaye aliipokea na kabla hajaelezwa
chochote, alisema alikuwa katika sehemu
ambayo asingeweza kuzungumza, hivyo
angempigia mwandishi wetu baada ya robo
saa.
JIDE VIPI?
Baada ya kukata simu, mwandishi wetu
alimwendea hewani Jide na baada ya kuita
kwa muda , simu yake ilipokelewa na Gardner
akasema : “ Mpigie baada ya robo saa . ”
DAKIKA 20 BAADAYE , GARDNER AFUNGUKA
Dakika ishirini baadaye, Gardner alimtumia
ujumbe mfupi wa simu mwandishi wetu na
kumweleza kuwa alikuwa Kituo cha Polisi
Oysterbay , Kinondoni jijini Dar ambako aliitwa
kwa ajili ya soo lao la kuwakimbia trafiki.
Baada ya kubadilishana maneno kadhaa,
baadaye aliamua kupiga na mazungumzo kati
yake na Ijumaa yalikuwa kama ifuatavyo ;
Ijumaa : Ebwana hivi hizi habari kwenye
mitandao juu ya kuvunjika kwa ndoa yako na
Jide zimekaaje ?
Gardner : Hamna kitu bwana, watu
wanaunganisha tu vitu sijui kwa sababu gani .
Ijumaa : Sasa kama ni hivyo kwa nini Jide
hakuja kukuona siku ile ulipolala polisi ?
Gadner: Unaona sasa, wao wanajua hivyo ,
lakini siyo kweli, Jide alikuja usiku sana kwa
sababu alikuwa anawaogopa mapaparazi .
Unajua Jide yeye huwa hapendi hayo mambo .
Alikuja usiku sana, lakini hata hivyo polisi nao
walimgombea sana kumpiga picha .
Ijumaa : Wanasema Jide kuna maneno
amepost kwenye akaunti zake mitandaoni
zinazoonyesha kuchoshwa na wewe,
unasemaje?
Gardner : Si ndiyo kama hivyo nimekuambia ,
watu wanaungaunga tu vitu ambavyo hawavijui
na sisi hata hatujui malengo yao .
Wakati ule uliponipigia simu mara ya kwanza
nilikuwa naye kwenye gari ananipeleka pale
polisi , lakini akapaki mbali kwa sababu
hiyohiyo niliyokuambia kuogopa mapaparazi
na si unakumbuka hata ulipompigia kwenye
namba yake nilipokea mimi ?
Ijumaa : Kwani upo naye hapo sasa hivi
nimsalimie ?
Gardner : Hapana tumeachana mimi niko
kwenye usafiri mwingine naelekea kazini na
yeye yupo kwenye misele mingine.
Ijumaa : Haya kaka basi poa.
Gardner : Poa kaka, mchana mwema .
HUKO NYUMA
Si mara ya kwanza kwa mastaa hao kudaiwa
kutibuana kwani walisharipotiwa kutaka
kutengana lakini mara nyingi huwa wanakaa
chini na kuyamaliza kimyakimya.