wa raia wa Ethiopia waliokamatwa
kwenye msitu wilayani Bagamoyo
wakituhumiwa kuwa wahamiaji haramu
na kulazwa hospitalini kutokana na
matatizo ya afya, amefariki akipatiwa
matibabu.
Dawita Alalo (25) ambaye alikuwa
miongoni mwa wahamiaji haramu 11
waliolazwa kwenye kituo cha afya cha
Chalinze, wilayani Bagamoyo, alifariki
juzi kwa ugonjwa wa malaria.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Pwani, Athuman Mwambalaswa alisema
Alalo alikuwa miongoni mwa raia 48 wa
nchi hiyo walioingia nchini isivyo halali.
Walikamatwa Agosti 22 mwaka huu
wakiwa kwenye msitu wa Kijiji cha
Visakazi Ubena Zomozi tarafa ya Chalinze.