Kwa mujibu wa Daily Mail, Waumini wa Hindu wanaamini kwamba Ng'ombe ni mnyama aliyebarikiwa na wanasema mkojo wake unasaidia kuponya vitumbalimbali.Japokuwa wanasisistiza kwamba mkojo wa ng'ombe unaotakiwa kunywewa ni ule wa ng'ombe bikira - ambaye hajawahi kuzaa. Pia, mkojo unatakiwa kuchukuliwa kabla ya jua kutoka na hapo ndipo mkojo huo unapokuwa na matokeo mazuri.Pia wamesema kwamba kunywa mkojo wa ng'ombe ndio njia bora ya kuondoa vipara kwenye kichwa.
Angalia picha hapo chini..
Jairam Singhal, 42, ambaye amekuwa akinywa mkojo wa ng'ombe kwa zaidi ya muongo mmoja ametoa ushuhuda juu ya faida za kiafya zinazosababishwa na mkojo huo::
‘Nilikuwa na kisukari, ila toka nimeanza kunywa mkojo wa ng'ombe, kiwango cha kisukari nimeweza kukikabili. Mtu mmoja aliniambia kunywa mkojo wa ng'ombe ni mzuri kwa afya. Tumekuwa na ng'ombe hapa kwa zaidi ya miaka 12, hivyo kitu cha kwanza kukifanya asubuhi ni kuchukua mkojo wa ng'ombe na kuunywa.’
Cheki picha zaidi hapo chini...