Muziki wa bongofleva umefanya mapinduzi sana kuanzia mwanzoni mwa miaka 2000 mpaka sasa, zifuatazo ndizo nyimbo bora za bongofleva zenye ujumbe ambazo hupaswi kuacha kuzisikiliza...
1. Dunia Njia,
hii nyimbo iliimbwa na Bushoke ni moja ya nyimbo zenye ujumbe mzito kabisa , ukiiskiliza anaelezea maisha kwa ujumla, maisha baada ya kifo na matabaka yaliyomo katika jamii,..hupaswi kuacha kuisikiliza hii nyimbo itakufunza mambo mengi
2 Kazi Yake Mola,
hii nyimbo imeimbwa na madee akishirikiana na mandojo na domokaya, kazi yake mola ni nyimbo inayohuzinisha kwa upande mmoja ila inafunza mambo mengi mnoo
3 Siku Hazigandi,
Malkia wa muziki wa bongofleva Jide akiwa katika ubora wake aliachia hichi kibao murua kabisa, achilia mbali midundo inayopatikana humu, ujumbe unaopatikana ni mkubwa sana unalenga kumfanya msikilizaji ajifunze kutokata tamaa katika maisha....
4 Ndio Mzee,
Professor J akiwa katika ubora wake alitunga hichi kibao ambacho kinakuelezea mustakabali mzima wa siasa na demokrasia ya kiafrika kwa kutumia lugha ya kiswahili, hii nyimbo inakufanya upate utashi mkubwa sana wa siasa za kiafrika na Tanzania....namshukuru Mungu nimebahatika kuisikia hii nyimbo
5 Darubini Kali,
Afande sele akishirikiana na Dogo ditto walitoa hichi kibao kilichomfanya Afande sele kuwa mfalme wa rhymes, kaongelea mambo mengi sana humu , ni moja ya nyimbo bora kabisa kuwahi kutungwa nchini Tanzania
6 Alikufa kwa Ngoma
Mwanafalsafa akishirikiana na Jide walitoa hichi kibao katika kipindi ambacho gonjwa la ukimwi lilikuwa tishio mno, aina ya ujumbe na uwasilishwaji wake kunaifanya hii nyimbo kuwa ya tofauti miongoni mwa nyimbo zote zilizokuwa zinaongelea kuhusu ukimwi,,,, hupaswi kuacha kutoiskiliza hii nyimbo
7 Mapenzi Kitu Gani,
huwezi ukazungumzia maisha ya mwandamu bila kuhusisha na mapenzi, MB DOGG akiwa katika ubora wake aliachia hichi kibao kujaribu kuonyesha uwalakini wa neno mapenzi, uhusiano wa utajiri, umaskini, umaarufu na mapenzi...ujumbe japo ni wa mapenzi lakini ni mzito mno....ni moja ya nyimbo bora kabisa za mapenzi hapa Tanzania
8 Elimu Dunia,
Daz baba aliachia kibao hichi ambacho ndani yake ujumbe wake unalenga kufundisha umuhimu wa elimu, hii nyimbo ni nzuri mno hupaswi kuacha kuisikiliza..
9 Sihitaji marafiki,
Farid kubanda nyimbo zake zote zina ujumbe mkali, ila ujumbe unaopatikana katika hii nyimbo ni wa kitofauti na wa kipekee,, kama nyimbo inavyojieleza "sihitaji marafiki'.......
10 Hii ndiyo Tanzania
Unataka kufahamu mambo ya Tanzania basi nenda kaisikilize hii nyimbo ya Roma mkatoliki inayoitwa "hii ndiyo Tanzania".........utapata ujumbe mzit sana aseee
Nadhani hizi ndizo nyimbo muhimu zaidi kwa Mtanzania yeyote kuisikiliza ....kama kuna ambayo imesahaulika au unalist yako hebu itaje hapa tuijadili.
Milioni 392 Zajenga Barabara HEWA Dar es Salaam
-
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob amebaini matumizi ya Sh392
milioni zilizoandikwa kwenye taarifa ya manispaa hiyo kuwa zimetumika kwa
ajili y...