Kanye West alikuwa kwenye tamasha lake nchini
Australia wakati huu na aliamua kuweka msimamo
kwa maneno aliyoyasema kuwataka mashabiki
wote kusimama na kucheza wakati anaimba la
sivyo asingeendelea na show.
“'I can't do this song, I can't do this show until
everybody stand up. Unless you got a handicap
pass and you get special parking and s**t.'Imma
see you if you ain't standing up, believe me, I'm
very good at that.”. Alisema.
Kwa bahati mbaya zoezi hilo lilikuwa gumu kwa
mashabiki wawili waliokuwa wamekaa kwenye kiti
maalum cha kuwasaidia kutembea na huenda
walikuwa walemavu ama wagonjwa wa miguu.
Kanye alisimamisha zoezi la kuimba ingawa watu
waliendelea kumpigia kelele wakimuonesha ishara
kuwa watu hao walikuwa kwenye wheelchairs.
Rapper huyo hakuamini maneno tu na alimtuma
mlinzi wake aitwae Pascal kuhakikisha na
kumletea majibu.
Pascal aliporudi alimhakikishia kuwa kweli
walikuwa kwenye wheelchairs na ndipo alipolegeza
masharti na kuendelea na show.
“He is in a wheelchair? It’s fine!” Alisikika Kanye
West.