Featured Posts

Saturday, September 13, 2014

Ali Kiba aeleza jinsi ambavyo Diamond alimkwaza, 'alikuwa ameconcentrate sana katika kunifunika'

Mwanamuziki wa Bongo Flava, Ali Kiba
amefunguka kuhusu mambo yaliyomkwaza kutoka
kwa Diamond miaka michache iliyopita baada ya
mkali huyo kutoka na wimbo wa ‘Kamwambie’
uliogeuka kuwa wimbo wa taifa wa Bongo Flava
kwa muda.
Akiongea na kipindi cha Mkasi, Ali Kiba ameeleza
kuwa yeye ndiye mtu aliyepitisha ombi la Diamond
kurekodi katika studio za SharoBaro kwa kuwa
wakati huo alikuwa mdau mkubwa katika uongozi
wa studio hizo lakini matokeo yake yalimgeukia
hadi kuamua kujitoa katika team hiyo.
Ameeleza kuwa mara baada ya Diamond kutoka na
Kamwambie, aliona gazeti moja lililokuwa
lililomkariri akisema kuwa yeye ndiye ‘fimbo’ ya
Alikiba na amekuja kumfunika.
Hata hivyo maneno yaliyowekwa kaitika gazeti hilo
yalianza kuaminika kwa Ali Kiba baada ya kukutana
nae mara kadhaa kwenye shows.
“Lakini nilishawahi kukaa na Diamond katika
mikutano ya Shows ambazo tunaitwa pamoja
wasanii na nini na nini. Mimi napendaga kuongea
nae kama mdogo wangu kwa sababu the way
nilivyokuwa nikimtreat ni kama wadogo zangu
wengine akina Bob Junior akina nani… Nilimsikia
akiongea sana kwamba nimekufunika kwenye show
fulani, nimekufunika kwenye show fulani. Kwa kweli
the way nilivyokuwa nikimtreat kama mdogo
wangu. Kwa hiyo yeye alikuwa ameconcentrate
sana katika kunifunika.” Alieleza Ali Kiba.
“Mimi sio mtu wa kumind sawa. Kwa hiyo
alivyokuwa anaongea anajifurahisha. Hata kama
amenifunika mimi nilikuwa naweza kumpigia
makofi vilevile. Si nataka afanikiwe. Kwanza
nafurahi. Napenda sana challenge. Inakufanya
unaaamke.” Aliongeza.
Kujirudia kwa neno ‘kufunika’ kila walipokuwa
akikaa na Diamond kuligeuka kuwa kero kwa Ali
Kiba huku mengine yakipenya kutoka kwa watu
wake wa karibu.
“Kwa hiyo kitu ambacho kilikuwa kinahappen
tukiwa karibu hivi, ni hivyo vitu ambavyo
akizungumziwa nimekufunikaa..nimekufunika.
Nikawa nikitoa video nasikia maneno, kwamba ‘Ali
amesikia maneno nimetoa hii na yeye ametoa hii’.
Mi sijawahi kumsikia mwenyewe akisema. Ila watu
wake wa karibu wa karibu wanakuja wanasema.
Unaweza kumjua mtu tabia yake kwa kumuangalia,
kwa kuishi nae.”
Ali ameeleza kuwa hata baada ya kuamua kukaa
kimya amlee mwanae wa kiume alisikia tena
maneno kutoka kwa mwimbaji kwa Diamond kuwa
amemkimbia.
Hata hivyo, hii ilikuwa story ya zamani ambayo
wengi wanaweza kuwa nayo lakini ikamhusu mtu
ambaye kwa sasa amekuwa rafiki wa kudumu.
Hivi karibuni Ali Kiba alisema kuwa hana tatizo
lolote na Diamond na kuwataka watu
wasimgombanishe na msanii huyo.
Ni muda wa biashara. Yaliyopita si ndwele
(maradhi) tugange yajayo kwa maendeleo ya
Bongo Flava. Kilichobaki ni ushindani wa
kibiashara kama alivyosema Babu Tale.

TUMEAMIA HUKU