Featured Posts

Sunday, September 7, 2014

AY apendekeza kiwango bora cha show wanachopaswa kulipwa wasanii wakubwa Tanzania

Malipo ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya
Tanzania katika shows ni sehemu ya kilio cha
wasanii hao ingawa wapo wachache wanaotangaza
kuneemeka na kipato hicho.
Akiwa katika Maskani ya 100.5 Times Fm na
Gardner G Habash, msanii wa kimataifa Ambwene
Yesaya amependekeza kuwa wasanii wakubwa wa
Tanzania (A-List) walipwe wastani wa shilingi
milioni kumi na tano (15,000,000) kwa show moja
ili kukuza zaidi kiwanda cha muziki.
AY ameeleza kuwa endapo wasanii wakubwa
watalipwa vizuri itakuwa nafasi nzuri ya wao
kuongeza nguvu na kufanya show nzuri zaidi ili
waongezewe kipato na wasishuke. Lakini pia
kiwango hicho kitawahamasisha zaidi wasanii walio
katika madaraja mengine ya chini kuongeza bidii ili
kufikia kiwango hicho.
Ameongeza kuwa endapo wasanii watakuwa
wanalipwa vizuri watatoa ajira zaidi kwa watu
wengine wakiwemo dancers, wauzaji wa nguo za
shows, watu wa back vocals, wasaidizi binafsi na
wengine.
Hivi sasa msanii anaelipwa kiasi kikubwa zaidi kwa
shows za ndani ni Diamond Platinumz. Kwa mujibu
wa meneja wake, Babu Tale hawafanyi shows
nchini bila Tsh. 15,000,000.
Hata hivyo kiwango hiki kina utofauti mkubwa na
viwango vya wasanii wengine wakubwa nchini
wanaofanya shows za nyumbani.
Kipindi cha Maskani cha 100.5 Times Fm kinakuwa
hewani Jumatatu hadi Ijumaa saa kumi kamili jioni
hadi saa moja kamili na huongozwa na Gardener
G. Habash.

TUMEAMIA HUKU