Yaliyomtokea Miss Tanzania 2006,
Wema Sepetu mwaka jana huenda
yakajirudia mwaka huu baada ya
kugundilika mahusiano mapya baina
ya Diamond na msanii wa muziki
aina ya Afro Pop na mtangazaji wa
kipindi cha Dance 100%
kinachorushwa kupitia kituo cha
Televisheni ya vijana EATV, Menina
Atick a.k.a Menina la Diva…..
Taarifa toka vyanzo vya kuaminika zinadai
kuwa Menina hivi sasa ndo binti pekee
aliyeiteka akili ya Diamond kuliko wote
waliowahi kuwa naye kimahusiano huku mama
mzazi wa Diamond Bi, Snura Kassim
akionekana kumkubali kwa asilimia zote binti
huyo….
Vyanzo hivyo vimebainisha kuwa mahusiano
ya Menina na Diamond yamekuwepo kwa
miezi kadhaa sasa na Diamond amekuwa na
wivu wa kupindukia juu ya demu huyo kuliko
inavyosemekana kwani amekuwa akimfuatilia
kwa kila hatua….
“Hakuna kitu anachokifanya Menina kwa sasa
Diamond asijue, anampenda vibaya utadhani
karogwa na kuna kipindi Diamond alitaka
kumzuia asijihusishe na chochote kwenye
Dance 100% kwa kuhofia kuporwa lakini
baadae alikubali aendelee na Dansi 100%
baada ya kuhakikishiwa na dada yake Queen
Darling ambaye ni mmoja wa majaji katika
shindano hilo kwamba atamlinda asiguswe na
mtu,” kimesema chanzo hicho.
Habari zaidi zinasema kwamba hata hivi majuzi
( kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani)
Wema alipigwa marufuku kushiriki maandalizi
ya futari nyumbani kwa kina Diamond kwa
kigezo kuwa taratibu za dini ya kiislamu
haziruhusu hawara kumpikia mwanaume futari
lakini Menina alikuwa akifanya jambo hilo kwa
kujinafasi….
“Karibu mwezi mzima Menina alikuwa akienda
kwa kina Diamond na kupika futari, mbali ya
hilo alikuwa akifanya kila alichokitaka katika
nyumba hiyo pamoja na kufanya usafi katika
chumba cha Diamond,” kimesema chanzo
chetu.
Hata hivyo chanzo chetu kimesema kuwa
kuna wakati Diamond aliwahi kusikika akisema
kuwa hawezi kumuoa Wema kutokana na
rekodi yake ya kuwahi kuwa na mahusiano
na watu wengi wanaojulikana nchini hivyo
kuwa naye kwa ajili ya kujitangaza kimuziki(
kumpatia kiki) tu na muda wa kuoa
utakapofika, ataoa binti asiye na umaarufu
jijini…..
Kibaya zaidi ni kwamba mama Diamond
ameelezwa kuwa na mapenzi ya dhati na
Menina jambo ambalo linamfanya akose raha
pindi Wema anapofika nyumbani kwake…
Diamond alipotafutwa kupitia simu yake ya
mkononi ili kuzungumzia jambo hilo, simu
yake iliita bila kupokelewa. Wema hakupatikana
katika simu zake zote.