“Karibu mwezi mzima Menina alikuwa akienda
kwa kina Diamond na kupika futari, mbali ya
hilo alikuwa akifanya kila alichokitaka katika
nyumba hiyo pamoja na kufanya usafi katika
chumba cha Diamond,” kimesema chanzo
chetu.
Hata hivyo chanzo chetu kimesema kuwa
kuna wakati Diamond aliwahi kusikika akisema
kuwa hawezi kumuoa Wema kutokana na
rekodi yake ya kuwahi kuwa na mahusiano
na watu wengi wanaojulikana nchini hivyo
kuwa naye kwa ajili ya kujitangaza kimuziki(
kumpatia kiki) tu na muda wa kuoa
utakapofika, ataoa binti asiye na umaarufu
jijini…..
Kibaya zaidi ni kwamba mama Diamond
ameelezwa kuwa na mapenzi ya dhati na
Menina jambo ambalo linamfanya akose raha
pindi Wema anapofika nyumbani kwake…
Diamond alipotafutwa kupitia simu yake ya
mkononi ili kuzungumzia jambo hilo, simu
yake iliita bila kupokelewa. Wema hakupatikana
katika simu zake zote. Rafiki huyo amesema kuwa kutokana
na jeuri ya pesa ya kigogo huyo,
Penny anatarajia kufanyiwa bonge la
harusi na watafanya kila namna ili
Diamond awe mtumbuizaji katika
sherehe hiyo….
“Huko kwao Johnson anamiliki migodi
zaidi ya kumi ya Almasi na yupo hapa
nchini kwa ajili ya uwekezaji, anampenda
sana Penny na ameahidi kumfanyia kila
atakacho,” alisema msichana huyo.
Baada ya kupata umbea huo,
Mwandishi alimtafuta Penny kupitia
simu yake ya mkononi na kumhoji
juu ya taarifa hizo ambapo alikiri
kuwa na mchumba na kusema ndoa
iko karibuni. “Nimeshakuwa sasa, hivyo nahitaji
kuolewa, ni kweli nina mchumba na ni
raia wa Angola, Inshaaalah Mungu
akipenda mambo mazuri yanakuja,
ntakutaarifu,” alisema Penny
Alipoulizwa kuhusu Diamond
kutumbuiza kwenye harusi yake, Penny
alijibu;
“Kutakuwa na wasanii wengu tu sasa
na yeye kama atapokea mwaliko wa
kuja kutubuiza atapatiwa nafasi, akiona
vipi, halazimishwi.”