Featured Posts

Wednesday, August 13, 2014

KENYA YAKABIRIWA NA HATARI YA, KUPATA, EBOLA

Shirika la afya duniani, limetahadharisha kuwa
Kenya inaweza kuwa katika hatari ya kukumbwa
na ugonjwa wa Ebola, kutokana na kasi ya kuenea
kwa ugonjwa huo.
Hatari hii inatokana na Kenya kuwa kitovu cha
usafiri wa ndege huku wasafiri wengi
wanaokwenda Afrika Magharibi wakipitia nchini
humo.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa onyo ya afisaa mkuu
wa shirika la afya duniani WHO.
Hili ndilo onyo kali zaidi kuhusiana na ugonjwa wa
Ebola kutolewa na shirika la WHO kwamba Ebola
huenda ikaenea katika kanda ya Afrika Mashariki.
Wataalamu wa afya wanasema kwamba
wanajitahidi kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo
Afrika Magharibi, ambako zaidi ya watu 1,000
wamefariki.
Canada imesema kwamba itatoa mchango wa dozi
1000 za chanjo ya majaribio ya Ebola kusaidia
watu kutoambaukizwa ugonjwa huo.
Kisa cha kwanza cha Ebola,kiliripotiwa nchini
Guinea mwezi Februari kabla ya kuenea hadi
nchini Sierra Leone na Liberia.
Nigeria ni nchi yenye idadi kuwba ya watu barani
Afrika na ndio ya hivi karibuni kuripoti kuwa na
thuluthi moja ya vifo kutokana na Ebola.
Kisa cha tatu kiliripotiwa siku ya Jumanne.
Mkurugenzi wa shirika la afya duniani tawi la
Kenya, Custodia Mandlhate, amesema kuwa nchi
hiyo iko katikahatari kubwa ya kupata Ebola. Hatua
za kuzuia maambukizi na kuweza kutambua
wagonjwa zimeshika kasi mjini Nairobi katika siku
za hivi karibuni.
Serikali hata bhivyo imesema kuwa haitasitisha
safari za ndege kutoka katika nchi nne
zilizokumbwa na ugonjwa huo Afrika Magharibi.
"Hatushauri, safari za ndege kusitishwa kwa
sababu ya mipaka yetu ambayo watu wanaingia na
kutoka pasipo vikwazo vingi, '' alisema waziri wa
afya James Macharia.
Kenya hupokea zaidi bya safari 70 za ndegekuoka
Afrika Magharibi.
Shirika la kikanda la Ecowas, limesema kuwa
mmoja wa maafisa wake Jatto Asihu Abdulqudir,
mwenye umri wa miaka 36, alifariki kutokana na
Ebola nchini Nigeria.

TUMEAMIA HUKU