habari wakidaiwa kuchochea kuni kwa namna moja
au nyingine.
Diamond Platinumz ambaye ndiye msanii
anaekabiriwa na ushindani mkubwa zaidi kwa sasa
kwa kuwa yuko mstari wa mbele zaidi wa
mafanikio katika muziki hapa nchini na kuvuka
mipaka kuiwakilisha Tanzania, amewashauri
wasanii wanaotaka kushindana nae kutojikita katika
ushindani wa nyumbani.
Diamond alifunguka katika mahojiano aliyofanya na
The Jump Off ya 100.5 Times Fm na Jabir Saleh
kabla hajapokea tuzo ya AFRIMMA kama mwimbaji
bora wa kiume Afrika Mashariki.
“Tutanue mawazo, tuache mawazo ya kushindana
wenyewe kwa wenyewe Tanzania. Labda kuleta
mabadiliko yataleta mabadiliko ya Chalinze,
mababadiliko ya Dar es Salaam au wapi.
‘Tukakomeshana tukikutana kwenye show labda ya
Mwembe Yanga,’ tuache hizo fikra.” Alisema
Diamond.
“Kwa sababu sisi tunaweza tukafikiri hapa kuna
pesa nyingi sana lakini hakuna pesa nyingi kama
ukifirikia kule mbele. Kwa sababu mbele unaweza
kupiga show mpaka dola 100,000 ambayo ni kama
milioni 160 au 170. And that’s the only way we
can make a lot of money.
“Nafikiria huu ni wakati wetu sisi, tufocus sasa na
mbele kuliko kufocus hapa tunakuwa tunabishana
sehemu ambayo ni padogo. Hapa tu kwenye
chumba kimoja tunang’ang’ania humuhumu, huyu
kashika mlango hatoki…wakati huku kuna sebule
kuna nini…” Aliongeza.
Mkali huyo wa MdogoMdogo ameeleza kuwa
wakati akiwa katika tuzo za BET alikuwa anaona
jinsi ambavyo baadhi ya watu walivyotengeneza
makundi na kuanza kumdiss bila sababu. Lakini
yeye kwake hiyo huwa inampa nguvu zaidi ya
kuwaza kuwa ni muda wa kuwakomesha kwa kutoa
vitu vikali zaidi.
Msikilize ha