Featured Posts

Monday, August 11, 2014

DAH HII NI LAANA. MTOTO WA MWAKA MMOJA ABAKWA NA NJEMBA. SOMA HAPA KUJUA. MKASA HUU

wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja
tunayemtaja kwa jina moja la Devota wa
Sokoni One jijini Arusha, amelazwa katika
Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru
kufuatia kubakwa na njemba moja
iitwayo Rajabu Mkoba (30), mkazi wa
eneo hilo.
Tukio hilo lilitokea Jumapili ya Agosti 3,
mwaka huu ambapo mtuhumiwa huyo
anadaiwa kumbaka mtoto huyo kwa saa 9
na alimrejesha nyumbani kwa mama yake
usiku wa manane.
Akizungumza na Ijumaa, mama wa mtoto
huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la
Mwitango alisema siku ya tukio, asubuhi
alimkabidhi mtoto wake kwa jirani yake
aliyemtaja kwa jina la Mustafa Kabananga
na yeye kwenda kwenye kikundi cha
akina mama.
Usiku saa mbili alikwenda kwa jirani yake
huyo kumchukua mtoto wake lakini
akaambiwa alichukuliwa na Rajabu.
“Nilikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa,
yeye anaishi na wazazi wake. Hata hivyo,
sikumkuta mwanangu wala mtuhumiwa,
nikarejea nyumbani.
“Lakini kabla sijarudi, nilimwambia mama
wa mtuhumiwa kuwa mwanaye kaondoka
na mtoto wangu akaniambia nirudi
nyumbani nikaendelee kumtafuta nikimkosa
niende kwake ili akajue cha kufanya,
aliamua kwenda polisi’’ alisema mwanamke
huyo.
“Ilikuwa saa 9 usiku nikiwa narejea
nyumbani kutoka polisi, nilimkuta mama
mzazi wa mtuhumiwa akiwa na mtoto
wangu akimrejesha kwangu lakini
mtuhumiwa hakuwepo.
“Niliamua kumchunguza vizuri mwanangu
ndipo nilipogundua kuwa sehemu zake za
siri zimevimba kupita kiasi huku damu
zikimtoka.
“Nilikwenda kumweleza mama yake jinsi
mwanaye alivyomtenda mtoto wangu na
kumwachia mtoto ampeleke hospitali,
alinisihi nisitoe taarifa za tukio hilo popote
na akaniahidi kunipa shilingi laki moja,”
alisema mama huyo.
Imeelezwa kuwa mama wa mtuhumiwa
baada ya kukabidhiwa mtoto huyo
hakumpeleka hospitali badala yake
alikuwa akimtibu kwa kutumia miti
shamba.
Baadhi ya majirani walikerwa na kitendo
cha mwanamke huyo ambapo
walimvamia na kumtolea maneno makali
ya kumtaka alifikishe suala hilo kwenye
vyombo vya sheria.
Kufuatia kelele za majirani ndipo
alipokubali kurudi Kituo cha Polisi cha
Unga Ltd ambapo polisi walifika
nyumbani kwa mama wa mtuhumiwa na
kumchukua mtoto huyo kisha
kumwandikia hati ya matibabu (PF3) na
kumpeleka mtoto huyo katika Hospitali ya
Mount Meru ambako anatibiwa.
Polisi hao walifungua jalada la mashtaka
la kubaka na kunajisi lenye namba Ung/
RB/2473/2014, bado mtuhumiwa
hajakamatwa kwani alikimbia baada ya
tukio hilo lakini mama yake ameshikiliwa
kwa mahojiano .

TUMEAMIA HUKU