Msichana wa miaka 18, raia wa India aliyetajwa kwa jina la Mangli Munda amefunga ndoa na mbwa baada ya kulazimishwa na wazazi wake kufanya hivyo kwa imani kuwa atafukuza roho za kishetani na mikosi inayomsonga.
Mbwa huyo alitafutwa na baba mzazi wa mrembo huyo na kufanyika sherehe kubwa ikiwa na vitendo vyote vinavyofanywa na ya bibi harusi na bwana harusi kwa taratibu zao za ndoa.
Kwa mujibu wa Yahoo News, msichana huyo hakuwa na furaha kabisa na alieleza wazi jinsi alivyochukizwa na kitendo hicho, “Siifurahii kabisa hii ndoa.”