Ajuza mwenye umri wa miaka 80 alimpiga mwizi usoni mwake nchini Uingereza na kumuogopesha kiasi cha kutoroka.
Mwanamke huyo, alikuwa anamtembeza Mbwa wake katika mtaa wa Whitstable, Kent, wakati jambazi huyo alipomvamia. Alikuwa amevalia mavazi meusi yaliyokuwa yamefunuika kichwa chake.
Alipigana na jambazi huyo na kumgonga kinywani. Polisi mjini Kent wanasema kuwa wangali wanamsaka jambazi huyo