HISIA! Mrembo aliyetinga hatua ya Tano Bora ya Shindano la Bongo Star Search (EBSS) 2013, Maina Thadei ameibuka na kuelezea hisia zake kuwa anateswa na penzi la staa wa Bongo Fleva, Asilahi Isihaka ‘Aslay’.
Akizungumza na gazeti hili, Maina alisema kuwa ameshindwa kabisa kuzizuia hisia zake kwa bwa’mdogo huyo ambaye anatamba na wimbo wa Ya Moto na kusema yupo tayari kwa lolote.
“Kwa kweli ananinyima usingizi, namfikiria sana. Naanza kazi moja tu ya kumsaka na nikimkamata hatoki hapa kwangu, sitakubali,” alisema Maina.
Pia mwanamuziki huyo aliongeza kuwa, atakapokuwa karibu na Aslay anaamini watatengeneza ‘kapo’ nzuri ambayo italeta ladha pindi watakaposhirikiana kimuziki.