KW/RB/8441/2014 imemshikilia Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga kwa madai ya kuzichapa na Miss Tanga 1997, Mona Faraja ambaye pia ni mke wake na kumsababishia majeraha, Risasi Jumamosi lina ‘full’ stori.
Miss Tanga 1997, Mona Faraja anayedaiwa kujeruhiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga.
Ishu hiyo iliyonyakwa laivu na majirani ilijiri usiku wa Jumatano iliyopita maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar, nyumbani kwa Lundenga wakati wawili hao walipokuwa wamepumzika baada ya mihangaiko ya mchana kutwa.Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, wakiwa wanabadilishana mawazo, mara simu ya Lundenga iliita na ndiyo chanzo cha mtafaruku, upi huo?
TUJINGE NA CHANZO
Mtoa habari wetu alisema kuwa, tatizo lilikolea mara baada ya simu hiyo kuita mfululizo kwa namba ngeni iliyodaiwa kuwa ni ya ‘kichenchede’ cha pembeni huku bosi huyo akiwa hana mpango wa kuipokea.

“Mke wa Lundenga alikuwa na shauku ya kujua nani anayepiga simu ya mumewe muda huo na kwa nini mumewe haipokei lakini wakati akiendelea kujiuliza ndipo ikaingia meseji ambapo inadaiwa Lundenga alikwenda ‘fasta’ kwenye inbox na kuifutilia kwa mbali.
“Kitendo cha kufuta SMS hiyo nacho kilitibua kabisa hali ya hewa, Mona akataka kujua kwa nini mumewe alikuwa hataki kupokea simu na SMS iliyoingia ilitoka wapi?
“Mona akawa mkali baada ya kuona haridhishwi na majibu ya mumewe ndipo alipoanza kutoa maneno yenye shutuma kwa mzee mzima ambapo naye uvumilivu ulimshinda kama binadamu wengine, wakaanza kutwangana,” kilisema chanzo hicho.

MKE AWAHI POLISI
Chanzo hakikuwa tayari kuweka ‘fullstop’, kiliendelea kumwaga mchele kwenye kuku wengi kuwa, baada ya mke kuona anazidiwa kwa kushushiwa makonde mazito yaliyomvimbisha uso, usiku huohuo alikimbilia Kituo cha Polisi Kawe, Dar kumripoti mumewe.

POLISI WAMKAMATA LUNDENGA
Mara baada ya mke kumaliza malalamiko yake kituoni hapo, saa chache baadaye polisi walifika nyumbani wakiwa na difenda ambapo walimchukua mlalamikiwa huyo hadi kituoni kujibu madai hayo.
“Polisi hawakuwa na maneno mengi, walipofika nyumbani walimkamata Lundenga na kwenda kumlaza kituoni kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria,” kilisema chanzo.

MAJIRANI WANENA
Baadhi ya majirani waliolitambua sakata hilo walionesha kushangazwa huku wakimhurumia Mona ambaye alikuwa ameumia usoni, hususan mzunguko wote wa jicho la kushoto.

MKE AINGIWA NA HURUMA
Wakati gazeti hili likiwa katika hatua za mwisho kuelekea mitamboni, Mona alidaiwa kuingiwa na huruma kwa kitendo cha kumlaza mumewe kituoni hivyo alikwenda kwa lengo la kumfutia mashitaka.

“Mke alimuonea huruma mumewe licha ya kupewa kipondo maana wamedumu kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 10 sasa, si mchezo. Alikwenda Kawe kufuta kesi lakini polisi wakamkomalia kwamba ishu lazima ifike mahakamani,” kilisema chanzo.
Mwandishi wetu alifika kituoni hapo na kukuta polisi na Mona wakiendelea na mazungumzo lakini hadi tunakwenda mitamboni, Lundenga alikuwa bado anashikiliwa kituoni hapo.
MKE WA LUNDENGA
Juzi, Risasi Jumamosi lilimpigia simu Mona kwa lengo la kutaka kumsikia anasemaje kuhusu madai hayo, lakini baada ya maelezo marefu ya mwandishi, alikata simu na baadaye kuizima kabisa!