Kanisa la mhubiri maarufu wa Nigeria, TB Joshua
linalojulikana kama The Synagogue Church of All
Nations limetoa tamko rasmi kuhusu tukio la
kuporomoka kwa jengo la ghorofa sita la kanisa
hilo, tukio lililoripotiwa kuua watu kadhaa na
kujeruhi, Ijumaa.
Katika tamko hilo lililowekwa kwenye ukurasa wao
wa Facebook, wamewakosoa waandishi walioripoti
kuwa kanisa zima limeporomoka na kwamba sio
kanisa wanalotumia kwa ibada bali ni jengo.
“Hili ni tamko rasmi kutoka The Synagogue,
Church Of All Nations kuhusu habari zinazoripotiwa
hivi sasa na vyombo vya habari kufuatia tukio
lililotekea leo. Ni jengo na sio kanisa (tunalotumia
kwa ibada) kama ilivyoripotiwa. Watu wachache
waliokuwa mule wameokolewa. Unachotaka kitokee
kwa wenzako, Mungu anakutakia wewe. Hakuna
kinachotufanya sisi kumpenda mtu kama
kumuombea. Kadiri navyokupenda, ndivyo kadiri
nitakavyokuombea.” Limesomeka tamko hilo.
Ingawa hawakuzungumzia kabisa kuhusu watu
kupoteza maisha au la..taarifa za awali zimeeleza
kuwa watu makumi wamepoteza maisha. Baadhi
ya mashuhuda walisema kuwa wameona miili ya
watu waliopoteza maisha ikitolewa katika jengo
hilo.