Featured Posts

Tuesday, September 9, 2014

PESA ZAZIDI KUMCHANGANYA KAJALA, AMWAGA MINOTI UWANJANIA, WATU WAPIGANA VIKUMBO KUOKOTA

FEDHA mwanaharamu! Katika hali ya kushangaza, staa wa filamu ambaye fedha imemtembelea kwa sasa, Kajala Masanja ‘K’ amenaswa akimwaga fedha kama amechanganyikiwa mbele ya kadamnasi, Risasi Mchanganyiko linakupa mchapo kamili.
Staa wa filamu, Kajala Masanja ‘K’ akiwatunza wakali kutoka Yamoto Band.
Tukio hilo lililowaacha watu midomo wazi lilitokea hivi karibuni katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar, kulipokuwa na uzinduzi wa filamu ya Mateso Yangu Ughaibuni ambapo muigizaji huyo alionesha jeuri ya fedha baada ya kupagawishwa na sebene la Yamoto Band.
ALIINGIA NA WAPAMBE
Awali, paparazi wetu alimshuhudia Kajala akitinga viwanjani hapo akiwa ameongozana na wapambe takriban 15 na kwenda kukaa katika meza moja ambapo mhudumu aliwasikiliza kujua wanachokunywa.
VINYWAJI VYAAGIZWA NJE
Kutokana na uzinduzi huo kutokuwa na pombe, K aliamuru kila mtu aletewe kile anachokihitaji halafu bili yote apelekewe yeye, Mama la Mama kama wanavyowaita watoto wa mjini.
“Waletee hawa vinywaji wanavyojisikia kunywa pia wasikilize meza ile pale kisha bili niletee mimi,” alisikika Kajala.
Mama wa Wamama 'Kajala' akirudi kukaa mara baada ya kuwatunza wakali wa Yamoto Band.
MINONG’ONO YAMTIA WAZIMU
Baada ya kauli ile wafuatiliaji wa mambo ya watu hasa wakienda shughulini wakaanza kutoa minong’ono kuwa hata iweje bado Kajala hajafikia uchezeaji wa fedha kama alivyokuwa shosti wake wa ‘long time’, Wema Sepetu aliyepewa taito ya Madam kutokana na kujua kuzitumbua fedha.
“Kwani kuagizia watu vinywaji ndiyo kuonyesha kufuru au jeuri ya fedha, angalia wahudumu wanavyogawa vinywaji kwa kusuasua, unafikiri angekuwa Madam (Wema) angekubali hata akae muda wote asiende kutunza thubutu, chezea Madame (Madam) wewe,” alisikika mualikwa mmoja.
Kajala akiserebuka na Mwanyekiti wa Bongo Muvi, Steven Mengere 'Steve Nyerere'.
YAMOTO BAND WAMWINUA
Ndani ya muda mfupi, Kajala akavunja ukimya baada ya bendi ya Yamoto kupiga wimbo wa Nitajuta ndipo Kajala aliposhindwa kuvumilia na kwenda kuwamwagia fedha huku wapambe wake wakimshangilia.
“Ndiooo mkurugenzi hivyo ndivyo ujana unavyoliwa,” kelele zilisikika kutoka katika meza waliyokuwa wameketi wapambe wake.
KAMA LAKI SITA NA USHEE
Ufukunyuzi wa paparazi wetu kwa harakaharaka, ulizihesabu fedha hizo alizowamwagia watoto hao wa Mkubwa Fella ambapo hesabu zilionesha zilikuwa zaidi ya shilingi laki sita.
Mama wa Wamama 'Kajala' akiwa na shosti yake 'Odama'
AKOSOLEWA
Hata hivyo kuna baadhi ya watu walimkosoa staa huyo kwa kusema kitendo cha yeye kupata fedha kwa sasa kinaonekana kumchanganya kiasi cha kuzimwaga pasipo kuwa na sababu ya msingi.
“Bora angetunza kidogo na nyingine akatumia kwa vitu vya maana likiwemo suala la kumsaidia mume wake ambaye yuko jela kwa kushindwa kulipa faini ya shilingi mil. 200,” alisikika mdau mmoja wa filamu ambaye hakutaka kuanikwa jina gazetini.
UZALENDO WAMSHINDA STEVE NYERERE
Kadri Kajala alivyozidi kumwaga fedha, uzalendo ulimshinda Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ambapo alimfuata Kajala na kutaka na yeye amtunze.
“Hebu kuwa na adabu, mi mkubwa wako na mimi nitunze kwanza mambo mengine yaendelee, haiwezekani uoneshe jeuri ya fedha kiasi hiki wakati mimi mdau nipo hapa hunipozi,” alisikika Steve Nyerere.
AMEZIPATA WAPI FEDHA?
Baada ya vurugu zote zile kufanyika, paparazi wetu alimvaa Kajala na kutaka kujua vyanzo vya fedha hizo na kumuuliza kama amehongwa, akachomoa.
“Mimi sihongwi ukitegemea fedha za mwanaume huwezi kuwa na heshima mjini, nina biashara zangu na kampuni yangu hiki ninachokitumia hapa ni faida tu ya siku mbili tatu mimi mjasiriamali wewe,” alisema Kajala.
TUJIKUMBUSHE
Kumbukumbu zinaonesha, kipindi ambacho Kajala na Wema walikuwa marafiki, Kajala hakuwa na fedha nyingi lakini baada ya kutofautiana, pesa imemtembelea huku mwenzake akidaiwa kuyumba kiuchumi.

TUMEAMIA HUKU