Tetesi za Beyonce kuwa mjamzito zimeendelea kusisitizwa hivi karibuni huku watu wake wa karibu wakieleza kuwa ameanza kufanya matendo kama aliyokuwa anafanya wakati ana ujauzito wa Blue Ivy.
Wikendi iliyopita, Beyonce alichochea tetesi hizo alipotembelea jumba la makumbusho ya kihistoria huko Ufaransa ambapo alikuwa ameshikilia tumbo lake kwa muda, huku likionekana kama limevimba kwa mbali.