Yaani kwa kweli mambo ya hii dunia ni ya ajabu na siku zote umdhaniae ndie kumbe sie kwa kweli, kuna rafiki yangu ambaye kwa kweli si kama tuna urafiki sana lakini ni rafiki maana tunaheshimiana nae sana na familia zetu zinafahamiana kwa kuwa tumejuana kibiashara na si mambo mengine.
Mme ndiye ambae ninafanya nae kazi ingawa mkewe namfahamu kwa kuwa ni sehemu pia ya msimamizi wa biashara za huyo mwanaume. Jana nilikua na appointment na rafiki yangu ambae ni daktari na ana hospitali yake.
Sasa wakati hiyo jana naingia nikakutana na huyo mdada ambae ni shemeji yangu, tuka salimiana nikamuuliza vipi hospital akasema ameenda kumcheki rafiki yake basi nikampotezea.
Sasa kumbe yule rafiki yangu dokta alituona nikiongea nae, nlipofika kuzungumza na dokta maana namjua tabia zake si za kistaarabu maana ni mdhaifu sana kwa wanawake, katika story akaniambia amemtoa mimba ya wiki3.
Jamani mimi nimempokea Yesu na nilimueleza dokta swala alilofanya ingawa ni rafiki yangu, lakini kitu kingine ni kwamba mume wa huyu dada yuko nje ya nchi tangu july 21 na atarudi mwishoni mwa mwezi huu kama mambo yataenda sawa ila hii inamaanisha mkewe si mwaminifu kwa ujauzito wa wiki3.
je, nina haja ya kumwambia awe makini na mke wake kwakua si mwaminifu?
By bomouwa