Featured Posts

Thursday, September 11, 2014

MASKINI MZEE MAGARI. ULE MCHEPUKO WAKE MATATA WAMKANA ,

Hamida Hassan na Gladness Mallya
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Faidha Omari ‘Sister Fay’ amedaiwa kumkana Charles Magali ‘Mzee Magali’ na kusema siyo baba yake halisi baada ya ndugu zake kumjia juu na kumtenga.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Faidha Omari ‘Sister Fay’
Kikizungumza na Ijumaa chanzo makini kilisema kwamba, Sister Fay amemkana Mzee Magali baada ya kubainika kwamba baba yake orijino alishafariki dunia siku nyingi.Baada ya kuzinyaka habari hizo mapaparazi wetu walimtafuta Sister Fay ambaye alisema: “Mimi nililelewa na mama tu, baadaye Mzee Magali alipojitokeza na kusema mimi ni mwanaye nikakubali.
‘Sister Fay’ akiwa kwenye picha ya pamoja na Mzee Magali.
“Lakini hivi karibuni ndugu zangu walijitokeza na kuniambia kuwa baba yangu alifariki hivyo kama nitaendelea kujiweka kwa Mzee Magali watanitenga, kwa hiyo naomba niseme kwamba Mzee Magali siyo baba yangu,” alisema Sister Fay.

TUMEAMIA HUKU