STAA wa filamu Bongo ambaye amejikita
kumtumikia Bwana kwenye wokovu , Ruth Suka
‘ Mainda ’ amesema kamwe hawezi kuainisha
sifa za mwanaume anayehitaji aolewe naye
kama ilivyo kwa mastaa wengine kwa kuwa
jukumu hilo ni la Mungu .
Staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘ Mainda ’ .
Akipiga stori na paparazi wetu, Mainda
alisema japo umri wake unaruhusu kuolewa
hawezi kuweka wazi sifa za mwanaume
anayehitaji awe wake kwa kuwa huenda sifa
anazozihitaji Mungu hajampangia kuolewa na
mtu wa aina hiyo .
“ Kwenye maono naona kabisa mume wangu
yupo karibu ambaye Mungu ameniandikia ,
sasa siwezi kusema nahitaji mwanaume
mwenye sifa zipi sababu nikisema nahitaji awe
hivi kumbe Mungu hajanipangia huyo, ”
alisema Mainda .