Featured Posts

Wednesday, September 17, 2014

KAGERA:MWANAFUNZI AJINYONGA KWA MADAI YA KUPEWA DAWA BILA VIPIMO

KAGERA:MWANAFUNZI AJINYONGA KWA MADAI YA KUPEWA DAWA BILA VIPIMO

Mwanafunzi wa kidato cha TANO katika shule ya sekondari ya IHUNGO, EZERA WABAMBA aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya mkoa wa KAGERA, amejiua kwa kujinyonga na shuka  kwa madai ya kukosa huduma sahihi za matibabu.

Akizungumza na waandishi  wa habari mkoani humo kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani KAGERA, GILLES MUROTO amesema marehemu kabla ya kujingonga aliandika ujumbe uliokutwa kwenye mwenye mwili wake ambao ulipatikana  baada ya maiti yake kufanyiwa upekuzi akieleza sababu zilizopelekea ajinyonge.
ujumbe huo ulisema haiwezekani binadamu kuhudumiwa kama mbwa ,huku akisema  amepewa dawa bila kufanyiwa vipimo
Kwa upande wake katibu wa hospitali hiyo JUSTUS BENGESI ambaye amethibitisha taarifa za kifo cha Mwanafunzi huyo, amesema si kweli kwamba amefikia uamuzi wa kujinyonga baada ya kukosa huduma sahihi za matibabu,na kuwa alifanyiwa vipimo vyote na kubainika akisumbuliwa na ugonjwa wa MALARIA.
Mwanafunzi huyo aliyejinyonga mwenye umri wa miaka 19 alikuwa mzaliwa wa TABORA na alikuwa akisoma mchepuo wa masomo ya SAYANSI.

TUMEAMIA HUKU