Tukio hilo lilitokea wiki iliyopita maeneo
ya Kawe jijini Dar es Salaam ambapo
wasanii hao walikuwa wakishuti video ya
wimbo wao unaokwenda kwa jina la
Tanzania ambapo walikuwa tilalila huku
mikononi wakiwa wameshikilia pombe
kali.
“Hii tunakunywa ili ipandishe stimu ya
kuimba kwani bila ya kuwa tilalila
tunakosa mzuka wa kuimba, unajua
ukitaka kuupatia muziki lazima uwe na
mzuka wa kutosha hivyo hapa tunashtua
ili kazi iende vizuri,” alisema Isabela.