Featured Posts

Saturday, September 20, 2014

DIAMOND.ARUDIA YALE YA UJERUMANI... ASHINDWA KUTOKEA KATIKA SHOW.LONDON UINGEREZA

Kwa mara nyingine tena , mashabiki wa
Diamond Platnumz wameshindwa kumuona
akitumbuiza licha ya kumsubiria hadi saa 10
Alfajiri.
Awamu hii imetokea jijini London , Uingereza
katika show aliyoitangaza kwa kiasi kikubwa
kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii .
Tofauti na Stuttgurt , Ujerumani ambako
mashabiki walifanya uharibifu mkubwa ,
mashabiki wa London waliamua kuwa wapole
tu na kurejea majumbani mwao na hasira
walizozimeza vifuani .
Chanzo cha Diamond kutotumbuiza kwenye
show hiyo kinaonekana kuwa ni kile kile kama
cha Ujerumani wiki kadhaa zilizopita yaani
promota kushindwa kumlipa fedha yake.
Staa huyo hakuchelewa kumtupia lawama
promota wa show hiyo , DJ Rule.
Akiweka picha ya promota huyo kwenye
Instagram, Diamond ameandika : Tafadhali
ndugu zangu wa UK !!! …. kuweni makini sana
na promoter huyu ( Victor – Dj Rule)
mnaposikia kaandaa show, party au hafla
yoyote…ni vyema kuziepuka na kutohudhuria
kabisa kwa sababu ni tapeli… . si unajua
aisifiae mvua imemnyeshea … basi miye
nimeloa kabisa.”

TUMEAMIA HUKU