Ajali imetokea leo mchana maeneo ya njia panda ya Ilala ambapo gari ndogo aina ya Toyota Rav 4 lenye namba za usajili T606 CHH liligongwa na Toyota DCM linalofanya safari zake kati ya Posta na Tabata Kimanga. Rav 4 ilifunga breki ghafla na basi likagonga kwa nyuma. Hakuna majeruhi wala mtu aliyefariki dunia.