Mapigano makali yaliyoendelea kwa siku mbili
mfululizo kati ya jeshi la Nigeria na wanajeshi wa
kundi la Boko Haram karibu na mji wa Michika na
Jumatatu ya wiki hii mtoto wa rais wa zamani wa
nchi hiyo, Olusegun Obasanjo alijeruhiwa.
Afisa wa serikali ya Nigeria ambaye hakutaka jina
lake litajwe, aliiambia Reuters kuwa mapigano hayo
makali yamehusisha mashambulizi ya ndege na
yaligusa maeneo ya Madagali, Bazza na Uba.
Mtoto wa Obasanjo, Lt. Col. Adebayo Obasanjo
alikuwa mmoja kati ya wanajeshi ambao
walijeruhiwa baada ya platoon anayoiongoza
kushambuliwa katika eneo la Bazza karibu na
Mubi, Adamawa siku ya Jumatatu.
Mtoto huyo wa Obasanjo alikimbizwa hospitali na
mapigano yakaendelea.
Hata hiyo, makao makuu ya jeshi la Nigeria
halijatoa maelezo zaidi kuhusu mapambano dhidi
ya Boko Haram katika siku ya Jumatatu na
Jumanne.
Kundi la Boko Haram linashikilia miji mbalimbali
yaliyo karibu na Borno lakini Jumatatu hii jeshi la
Nigeria liliweka kizuizi dhidi ya kundi hilo lilokuwa
likijitanua kuelekea kwenye miji mingine.