Akizungumza na Bongo5 leo, Mwasiti amesema
hana mpango wa kuolewa kwa sasa na wala hana
ujauzito kama watu wanavyozusha. “Nasikia eti
watu waniambia nina mimba, sina mimi na sijui
hizo habari watu wanazipata wapi,” amesema.
“Sina mpango wa kuolewa, vyote watu wanazusha
tu. Kweli hakuna mwanamke asiyetamani kuwa na
mtoto hata mimi napenda sema ni majaliwa,
mambo yote anapanga Mungu,” ameongeza.
Katika hatua nyingine Mwasiti amezungumzia ujio
wa wimbo yake mpya uitwao ‘Leo’ aliomshirikisha
Godzilla.
“Nina ngoma mbili ambazo ninategemea ziende
mtaani. Nina Leo ambayo nimemshirikisha Godzilla
halafu nina Kisigino ambayo nimeimba mimi peke
yangu lakini sijajua itatoka ipi, Nyimbo zote mbili
ni aina mbili tofauti za muziki. Muziki wa Mwasiti
wa sasa hivi upo kwelI leo, lakini kwenye Leo
tumeimba tofauti, mtashangaa kumuona Godzilla
ambaye amebadilika sio Godzilla ambaye
amezoeleka, ni Godzilla mwingine kabisa,
nimeamua kumbadilisha.”
“Kwahiyo ukisikiliza Leo utasikiliza ladha mbili
tofauti, utamsikia Godzilla na Mwasiti. Hiyo
tumefanya chini ya producer Chizan Brain, B
Records na Kisigino ni wimbo wa kuchezeka na
tumefanya na Shebby Records. Kwahiyo yoyote
kati ya hizo inaweza ikatoka lakini itaanza video
kwanza.”